SHIRIKA LA MAGEREZA LATILIANA SAINI MKATABA KATIKA SHUGHULI ZA KILIMO NA UFUGAJI NA MWEKEZAJI TOKA NCHINI UTURUKI, JIJINI DAR
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja( meza kuu mbele)
akisaini Mkataba wa Uwekezaji katika shughuli za Kilimo na Ufugaji na
Mwekezaji toka nchini Uturuki, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TARBIM
LTD, Bw. Baddal Calikusu(wa kwanza toka kulia). Hafla fupi ya
utilianaji saini Mkataba huo umefanyika Machi 17, 2014 Makao Makuu ya
Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam. Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja(mbele meza kuu)
akitoa utambulisho wa Makamishna wa Jeshi la Magereza(waliopo
kushoto)kwa Mwekezaji wa shughuli za Kilimo na Ufugaji kabla ya
kutiliana saini Mkataba wa Uwekezaji wa masuala ya Kilimo na Ufugaji
katika Shamba la Magereza lililopo Bagamoyo, Mkoani Pwani.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akibadilishana Mkataba
wa Uwekezaji katika shughuli za Kilimo na Ufugaji na Mwekezaji toka
Nchini Uturuki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya TARBIM LTD. Jeshi
la Magereza kupitia Shirika lake la Magereza limetiliana saini Mkataba
huo ambao utatekelezwa katika Shamba la Magereza lililopo Bagamoyo,
Mkoani Pwani.Mkurugenzi
wa Kampuni ya TARBIM LTD(kulia mbele meza kuu) akiagana rasmi na
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto mbele
meza kuu) mara baada ya hafla fupi ya utilianaji saini wa Mkataba wa
Uwekezaji katika shughuli za Kilimo na Mifugo ambapo Jeshi la Magereza
kupitia Shirika lake la Magereza litatekeleza miradi ya Uzalishaji ya
Kilimo na Ufugaji katika Shamba la Magereza lililopo Bagamoyo, Mkoani
Pwani kwa kushirikiana na Kampuni ya Mwekezaji ya TARBIM LTD(Picha zote
na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
EmoticonEmoticon