March 18, 2014

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YAWATAKA WANANCHI KUFUATA SHERIA NA TARATIBU

1 (11) 
Afisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Viwanda na Biashara Nicodemus Mushi, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukaguzi wa leseni za biashara kwenye ukumbi wa MAELEZO leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uhamasishaji wa Masoko wa waizara hiyo Christopher Mashingo.Kulia ni Afisa Habari Idara ya Habari (MAELEZO), Frank Mvungi.Picha na Hussein Makame-MAELEZO.

2 (7)Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uhamasishaji wa Masoko wa waizara hiyo Christopher Mashingo.Kulia ni Afisa Habari Idara ya Habari (MAELEZO), Frank Mvungi. Picha na Hussein Makame-MAELEZO.
3 (7)Waandishi wa Habari wakiwa kazini kwenye mkutano kati ya wawakilishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara (hawapo pichani) na waandishi hao, kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam leo. Picha na Hussein Makame-MAELEZO.
…………………………………..
Hussein Makame-MAELEZO
WIZARA ya Viwanda na Biashara imewataka wananchi kufuata sheria na taratiu za nchi katika kuendesha biashara zao kwani kufanya hivyo ni alama ya maendeleo na  kigezo kimoja cha kupima maendeleo ya watu ni  jinsi anavyofuata taratibu.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uhamasishaji wa Masoko wa wizara hiyo, Christopher Mashingo wakati akizungumza na waandishi wa habari ukaguzi wa leseni za biashara leo jijini Dar es Salaam.
Mashingo alisema Serikali ilirejesha utaratibu wa kupata leseni ya biashara kwa kulipia kuanzia Julai 1 mwaka jana na kutoa kipindi cha miezi 6 kwa wafanyabiashara waliokuwa na leseni zisizo na ukomo kuhuisha leseni zao.
Alisema kipindi hicho kiliisha Desemba 31 mwaka na wale waliochelewa kufanya hivyo walipata leseni zao kwa kulipa ada na adhabu kwa mujibu wa Sheria ya Leseni Namba 25 ya mwaka 1972 kifungu cha 11 (a) na (b).
“Wito kwa wananchi kufuata kufuata sheria na taratiu za nchi katika kuendesha biashara zao kwani kufanya hivyo ni alama ya maendeleo na  kigezo kimoja cha kupima maendeleo ya watu ni  jinsi anavyofuata taratibu”, alisema Mashindo.
Alisema ofisi yake inafanya ukaguzi ili kuhakikisha kuwa biashara zinafanyika kwa mujibu wa Sheria na Taratibu za nchi kama alivyoagiza Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara.
Aliongeza kuwa Katibu Mkuu huyo aliagiza kwamba Mamlaka za Leseni zifanye ukaguzi wa kina katika maeneo yao, na kusisitiza kuwa ukaguzi huo ufanyike kati ya mwezi April na Mei.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »