TAARIFA MAALUM YA POLISI MKOA WA DODOMA KUKAMATWA KWA MANAMKE LEO LIVE!!
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Dodoma kamishna msaidizi mwandamizi DAVID MISIME
(SACP) anawashukuru wananchi wa kondoa kwa jinsi walivyotoa ushirikiano
kwa Jeshi la Polisi na kufanikisha kumkamata mwanamke aliyeiba mtoto
mchanga wa siku moja tarehe 20.01.2014 huko katika maeneo ya Hospitali
ya Wilaya ya Kondoa.
Mtoto
huyo wa jinsia ya kiume alizaliwa tarehe 19.01.2014 huko katika zahanati
ya Thawi. Mama yake mzazi SALMA S/O ZUBERI, mpare, mkazi wa kijiji cha
Mwembeni, Kata ya Changaa - Kondoa, alipatwa na matatizo ambayo
yalimlazimu kuhamishiwa katika hospitali ya Wilaya ya Kondoa. Wakati
mama huyo akiwa anapatiwa matibabu na daktari alibidi mkwe wake aitwaye
HADIJA D/O SAID awe anambeba mtoto huyo mchanga. Alitoka naye nje na
ndipo akakutana na AMINA D/O JUMANNE MWASI, 22 Yrs, mkazi wa Mningani,
Kondoa mjini, alianza akuongea na nyanya wa kichanga hicho cha siku
moja baada ya kuzoeana na mwanamke ambaye alijieleza kuwa amelazwa hapo
hospitali kutokana na ujauzito aliomba kumshika au kumpakata mtoto
huyo.
Mama
mkwe huyo alitoka kwenda kutafuta chakula ili mgonjwa atakapomaliza
matibabu aweze kula. Baada ya muda alirudi akashangaa kutokumwona mama
ambaye naye alikuwa amejifanya ni mjamzito haonekani, alijaribu
kumtafuta maeneo mbalimbali na kuuliza watu mbalimbali bila mafanikio
ndipo akaamua kutoa taarifa Polisi.
Kwa
vile taarifa zilikuwa zimetolewa maenoe mbalimbali wananchi wema
walimtilia mashaka mwanamke aliyeiba mtoto na andipo kwa ushiriano
mkubwa baada ya kumfuatilia kwa karibu sana Polisi wakafanikiwa kumtia
mbaroni tarehe 29.01.2014 wakati alipompeleka motto huyo hospitali ya
Wilaya kwani mtoto alianza kuugua.
Baada
ya mahaojiano alikubali kuwa alimuiba mtoto huyo na hata uchunguzi wa
kitaalamu umebaini mwanamke huyo hajajifungua siku za karibuni.
Ninatoa
wito kwa wananchi kutokuamini watu wasiwafahamu kwa asilimia mia, hata
kama wanalugha nzuri kiasi gani pia nawatahadharisha wanawake waliokosa
watoto kwa muda mrefu utatuzi wake sio kuiba watoto wa watu wengine.
DAVID MISIME – SACP
KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA
chanzo blog ya wananchi.

EmoticonEmoticon