WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUTOANDIKA HABARI ZA UCHOCHEZI

January 30, 2014
Na Elizabeth Kilindi,Bumbuli
WAANDISHI   wa habari nchini wametakiwa kutoandika habari zinazochochea mifarakano katika jamii kwa misingi ya chuki,dini rangi au itikadi za kisiasa na badala yake watumie kalamu zao kuandika habari zitakazoleta  manufaa kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Diwani  wa  Kata  ya  Millingano,Hozza  Mandia wakati  akizungumza na TANGA RAHA BLOG  na kueleza kuwa waandishi wanatakiwa kuzingatia haki za pande zote mbili na kusisitiza uadilifu katika kutoa habari hizo.



Aidha aliwataka kujikita zaidi katika kuandika Habari hasa za vijijini kwani huko kunachangamoto nyingi ambazo hazijulikani au hazipewi kipaumbele kutoka na kutofikika kwa wakati hivyo huchangia kudumaza maendeleo kwa kutosikika kwake

“Nawataka kujikita zaidi katika kuandika habari za vijijini na za  unyanyasaji wa kijinsia hususani kwa watoto na wanawake kwani takwimu zinaonyesha hali sio nzuri katika kundi hilo la jamii kutoka na kugubikwa na usiri na pamoja na kuendeleza mila potofu “Alisema Hozza



Sambamba na hayo aliupongeza Muungano wa club za Waandishi wa HabariTanzania UTPC kwa kuendeleza weledi kwa wanachama wake kwakuwapatia mafunzo mbalimbali yenye lengo la kuboresha taaluma hiyo iendane na hali ya sasa kimaendeleo.



Aidha Hozza alisema licha ya kuwepo mapungufu ya hapa na pale lakini bado kuna waandishi wamekuwa wakitimiza majukumu yao ya kutoa habari kwa jamii bila kujali mapungufu hayo  kwa hali hiyo bado kunahitajika kuimarisha sekta hiyo ili iwebora zaidi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »