*TAMKO LA JOHN MALECELA KUHUSU WANAOJINADI KUWANIA URAIS 2015
Ndugu
zangu waandishi wa habari, awali ya yote naomba niwasalimie na
niwapongeze kwa kufika -mwaka mpya 2014, pia naomba niwapongeze kwa kazi
kubwa ambayo mmekuwa mkiifanya hasa kuhakikisha watanzania wanapata
habari kwa kila jambo linaloendelea kila kona ya taifa letu la Tanzania.
Ndugu
waandishi wa habari nimewaita hapa ili kuzungumza nanyi na mnisaidie
kufikisha ujumbe kwa watanzania hasa kuhusu jambo hili ambalo limekuwa
gumzo kwa watanzania wengi la mbio za urais 2015 kwa baadhi ya watu
ndani ya chama changu cha mapinduzi (CCM), kilichonisukuma zaidi na
kupata hamu ya kuongea nanyi ni baada ya kumsikia -na kumuona kijana
wetu ndani ya chama cha mapinduzi bwana Paul Makonda akiwa na ujasiri wa
kukemea vitendo mambo haya yanayofanywa na baadhi ya viongozi bila
uwoga wowote naomba tuchukue fursa hii kumpongeza sana kijana huyu.
Nadiriki
kusema nampongeza kijana huyu hasa kwa kauli zake nzito na za kijasiri
kwa maslahi ya chama changu cha CCM ili chama kiendelee kupendwa na
kuchaguliwa na watanzania.
Pia
itakuwa si busara kama sitawapongeza vijana wangu katibu mkuu wa chama
ndugu ABDULRAHMAN KINANA na NAPE NNAUYE kwa juhudi zao za dhati za
kujenga chama na kuendelea kuwaeleza wananchi juu ya misingi bora ya
chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuwakemea viongozi wasiofaa bila kujali
cheo na umaarufu wao ndani ya chama na serikali, nawaomba waendelee -na
juhudi zao hizo nami naziunga mkono juhudi zao na kama kuna watru
wanaowabeza naomba wasijali kwani kukemea viongozi wasiofaa ndani ya
chama na serikali ni msingi wa chama chochote kilichounda serikali.
Aidha nawaomba watanzania
wenzangu wazalendo wasikubali kukatishwa tama na kikundi cha watu
wachache wasio na mapenzi mema na taifa letu ambalo limekuwa mfano wa
kuigwa kwa amani, upendo, utulivu na mshikamano urithi tulioachiwa na
baba yetu wa taifa mwalimu julias kambarage nyerere ndani na nje ya
mipaka ya bara letu la afrika.
Ndugu zangu waandishi wa
habari naomba niwaambie kuwa msemaji wa UVCCM kijana wetu Paul Makonda
namuunga mkono kwa -kitendo chake cha ujasiri cha kumkemea ndugu EDWARD
NGOYAI LOWASSA bila uwoga kwa jinsi anavyokivuruga chama chetu kwa lengo
la kutaka urais 2015 huku secretariet ya chama ikiwa imekaa kimya
wakati inajua kuwa muda wa kuanza mbio hizi bado na kufanya hivi kwa
sasa ni kukiuka misingi na katiba -ya chama. Hapa najiuliza kuwa ile
misingi imara ya uongozi ndani ya chama chetu cha mapinduzi iko wapi?
Mpaka tumuachie mototo ndio akemee haya? Je, hapa chama kiko wapi?
Ukweli ni kwamba wanachama
wetu na vijana wamekuwa njia panda huku wakitamani kusikia tamko au
karipio la chama juu ya suala hili la harakati za urais 2015 bila
mafanikio.
Naomba niseme kuwa bila kuwa
na karipio au tamko la chama, hawa wanaotumia pesa zao hadharani kwa
lengo la kutafuta umaarufu na ushawishi kwa vijana ili kupata madaraka
wanaharibu misingi yetu bora ya uongozi iliyowekwa na waasisi wetu ndani
ya chama.
Kinachonisikitisha zaidi ni
kuona juhudu za uongozi wa sasa wa chama ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na
sekretarieti inayoongozwa na katibu mkuu ABDULRAHMANI KINANA na katibu
mwenezi NAPE NNAUYE za kutetea chama hiki zinatiwa mchanga.
Ninaomba juhudi hizi zisibezwe
na watu wenye nia njema na chama. Ukweli ni kwamba vijana hawa wamekuwa
na juhudi kubwa sana ya kujenga na kuimarisha chama chetu -kwa wananchi
kila pembe ya taifa letu kwa kukemea na kueleza misingi ya uongozi
bora. Swali: Je! Chama hakioni haya mpaka vijana ndio waone?
Kwa hili ni lazima tubadilike
ili kujenga chama chetu na naishauri -secretariet ya chama lazima
ichukue hatua mara moja, kijana huyu paul makonda asingesema haya yote
kama hana uhakika wa ushahidi wa wa haya aliyoyasema na nampongeza sana.
Vijana na wanachama wengi wa
CCM wamekuwa na hamu kwa muda mrefu ya kutaka kujua msimamo wa chama
chao bila mafanikio na ndio sababu ya baadhi ya-wengine kupoteza
mwelekeo.
Sisi tulikijenga chama hiki
kwa taabu sana hapakuwa hata mtu mmoja aliyediriki kutumia fedha zake
kutaka madaraka. Nidhamu, busara na uchungu wa rasilimali za taifa hili
kwa maslahi ya wananchi ndio vilituongoza kufuata misingi na maadili ya
uongozi ndani ya chama na serikali, ndio maana tunaumia sana kuona chama
sasa kinataka kutekwa na wenye fedha kwa uchu wa madaraka, mpaka
tunashangaa na kujiuliza hizi pesa wanatoa wapi? Na haya madaraka
wanayotaka kwa kununua ni kwa maslahi ya nani? Huku watanzania
wakiendelea kuwa maskini.
Mfano hivi karibuni baadhi ya
viongozi wa chama ngazi ya juu wamejibishana kwenye vyombo vya
habari,vitendo hivi havina tija kwa chama na wala havileti umoja na
mshikamano ambao umedumu ndani chama kwa muda mrefu.
Mwisho
Ninaomba sekretarieti ichukue hatua haraka kama alivyoomba kijana wetu
makonda na kweli kuchelewa kuchukua hatua jambo hili kumejionyesha wazi
kwamba utaleta kutokuelewana ndani ya chama kusiko kuwa na lazima.
JOHN SAMWELI MALECELA
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

EmoticonEmoticon