Na Elizabeth Kilindi,Muheza.
WAZEE wanaoishi kwenye kambi ya Ukoma Iliyopo Ngomeni
wilayani Muheza wameiomba serikali kuwajenga uzio kwenye kambi hiyo ili
kuwanusuru na vibaka wanaowavamia mara kwa mara na kupora mali zao ikiwemo
mifugo pamoja na ujenzi wa vyoo bora.
Ombi hilo wakati wakipokea Msaada wa nguo na chakula kutoka Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Tanga
wakati taasisi hiyo ilipo kwenda kutembelea kambi hiyo ili kubaini
changamoto zinazowakabili.
Aidha alisema kambi hiyo ipo mbali na makazi ya watu huku
wanaoishi ni wengi wao ni wazee hivyo inakuwa rahisi kwa vibaka na wezi
kuwavamia mara kwa mara hasa katika kipindi wanacho pelekewa misaada na
wasamaria wema kwama wao.
“Tatizo kubwa sisi tunaiomba serikali ituangalie katika swala
la kujengewe uzio na uhakika wa maji safi na salama kwani kwasasa hakuna
inatulazimu kwenda mwendo mrefu kutafuta maji huku hata bwawa lilichimbo kwa
ajili yetu limekauka kwa kukosa mvua”alisema
Mohamed Salimu.
Kwa upande wa Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mathew
Mganga alisema kuwa kambi hiyo inajumla ya wazee 86 ambao wanatumia matundu matatu ya vyoo ambayo hayaelingani na
idadi ya watu waliopo tu hali inayohatarisha usalama wa afya zao kwa ujumla.
Pia aliongeza kuwa
kwa sasa bajeti inayotolewa na Wizara ya Afya kwa kambi hiyo ni ndogo
licha ya Halimashauri kutenga mafungu kwa ajili ya kutatua matatizo madogo
yalikuwepo bado hali hasa miundombinu ya majengo sio ya kuridhisha.
Naye Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga Edson Makallo alisema kuwa iwapo
watendaji kwenye ngazi ngoze wangeweza kusimamia fedha za maendeleo na
kuhakikisha zinawafikia walengwa rushwa katika nchi hii ingepungua au kwisha
kabisa.
“Kwa kweli lengo letu ni kuhakikisha
tuwajibika katika kuwafikia wananchi wote na kutoa elimu kuhusu madhara ya rushwa
pamoja na kusimamia raslimali za maendeleozinasimamiwa ipasavyo ikiwa
kupunguza mianya ya rushwa katika huduma za kijamii”alisema Makallo.
EmoticonEmoticon