Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wanakijiji wa Mtanzania Januari 16, 2013 wakati alipokwenda kuwapa pole kufuatia uvamizi waliofanyiwa na watu wanaosadikiwa kuwa wafugaji ambao waliua watu watatu na kuchoma nyumba . Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Erasto Mbwilo.
Baadhi ya wananchi wa Kiteto wakimsikiliza Waziri Mkuu , Mizengo Pinda wakati alipowahutubia Januari 16, 2014 katika mji wa Kibaya alipokwenda kuwapa pole wakulima wa wilaya hiyo ambao walishambuliwa, kuuwawa na nyumba zao kuchomwa moto na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafugaji.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Kiteto baada ya kuwasili wilayani humo Januari 16, 2014 kufuatilia suala la mauaji ya wakulima
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na wazee wa Kiteto wakati alipoteta nao baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Kibaya Janauari 16, 2014. Alikwenda Kiteto kuwapa pole wakulima ambao walishambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafugaji ambao waliua na kuchoma moto nyumba.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na wazee wa Kiteto wakati alipoteta nao baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Kibaya Janauari 16, 2014. Alikwenda Kiteto kuwapa pole wakulima ambao walishambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafugaji ambao waliua na kuchoma moto nyumba. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
EmoticonEmoticon