March 03, 2014

MELI INAYOZUA MASWALI MENGI YASIYO NA MAJIBU KWA KUTIA NANGA PEMBENI MWA HOTELI YA KUNDUCHI BEACH

Katika harakati za jicho la Kamera ya Sufianimafoto, ilinasa 'Image' ya picha ya Meli hii pichani isiyokuwa na jina wa kiashilio chochote cha kuonyesha mahala inapotoka meli hii, jambo ambalo lisatengeneza maswali mengi yasiyo na majibu kwa kila atakayepata fursa ya kuiona meli hii ikiwa imetia Nanga eneo hili la nyuma ya Hoteli ya Kitalii ya Kunduch Beach, jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wadau waliozungumza na Mtandao huu, walisema kuwa meli hiyo ina muda mrefu sasa tangu walipoanza kuiona mahala hapo huku ikiwa haina shughuli yeyote zinazoendelea kwenye Meli hiyo wala mhusika.


Aidha imeelezwa kuwa Meli hiyo ni mali ya mfanyabiashara mmoja wa vyuma chakavu, ambaye ameinunua kusikojulikana na kuitelekeza mahala hapo, ambaye amekuwa akinunua meli kuukuu na kufanya shughuli ya kuzikatakata katika eneo hilo pembezoni mwa hoteli ya Kunduchi Beach na kisha kuuza vyuma chakavu.


Hakuna baya katika hili kutokana na kwamba ni biashara ambayo inafanywa na waliowengi kwa hivi sasa na wala si kosa la jinai, lakini kutokana na kitendo cha kuachwa mahala hapa kwa muda mrefu tena pembeni mwa Hoteli kubwa kama hii kinaacha maswali  mengi tu yasiyokuwa na majibu.

1. Kwa nini mmiliki wa meli hii achague eneo la hoteli za kitalii kufanyia chinja chinja ya meli chakavu?

2. Je zoezi hilo halina madhara au haliathiri mazingira kwa namna moja ama nyingine?

3. Mamlaka husika wana habari ya zoezi hili?

4. Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni ina habari juu ya zoezi la mfanyabiashara huyu katika eneo hili?

Hayo ni baadhi ya maswali na mengine mengi yasiyokuwa na majibu ya haraka. Jitihada za kumtafuta Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugwimbana ili kuzungumzia juu ya suala hili ziligonga ukuta baada ya kumtafuta kwa njia ya simu na muda wote simu ikiwa bize ikiita bila majibu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »