March 10, 2014
KADO:Amnyima raha Chippo:

MLINDA Mlango namba moja wa Klabu ya Coastal Union Shabani Kado mwishoni mwa wiki alimpa mawazo mazito Kocha Mkuu wa timu hiyo,Yusuph Chippo mara baada ya kuumia kwenye mechi yao na Ashanti United na kulazimika kutoka nje ya uwanja wakati mchezo huo ukiendelea.
Kado aliumia mara baada ya kukumbana na mshambuliaji wa Ashanti United Hussein Said na hivyo nafasi yake ilichukuliwa na mlinda mlango wa akiba Said Lubawa ambaye aliweza kulinda lango hilo mpaka mchezo huo unamalizika.

Baada ya kutokea hali hiyo,Chippo alikuwa na mawazo makubwa kuhusu mlinda mlango huyo huku akiwa kwenye bechi akiwa umeshika tama ikionekana kuumizwa na kuumia kwa mlinda mlango huyo.

Akizungumzia kuumia kwa kado mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo,Chippo alisema ana mshukuru mungu kuwa hakuumia sana hivyo ataweza kucheza mechi zinazofuata kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania bara.

  "Makipa wetu wote wana uwezo mzuri hivyo kuumia kwa kado sio maumizi makubwa sana  hivyo tunategemea atacheza kwenye mechi zetu zinazofuata "Alisema Chippo.

Akizungumza mchezo huo,Mwenyekiti wa timu hiyo,Hemed Aurora alisema kilichowafanya kushindwa kuchukua pointi tatu muhimu kwenye mechi yao na Ashanti United alisema walikuwa wameingia kwa hamasa kubwa na wachezaji wake kuwa na hali ya kujiamini sana.

Aurora alisema watahakikisha wanajipanga vizuri ili kuweza k ufanyavizuri kwenye mechi zao zinazofuata ili kuweza kujiweka kwenye nafasi za juu kwenye ligi hiyo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »