KIBADENI:TUTAPIGANA KUSISHUKE DARAJA LA LIGI KUU TANZANIA BARA.

March 10, 2014
KOCHA MKUU wa timu ya Ashanti United,Abdallah King Kibadeni amesema malengo yake makubwa kwenye timu hiyo ni kuhakikisha anapigana kufa na kupona ili kuweza kuibakiza timu hiyo kwenye daraja la Ligi kuu Tanzania bara.
Kibadeni alitoa kauli hiyo mara baada ya kumalizika kwa mechi yao na Coastal Union ambapo timu hizo zilitoka sare ya kutokufungana mchezo uliochezwa kwenye dimba la CCM Mkwakwani.



Alisema timu yao ilicheza kwenye kiwango cha chini kutokana na kuzoea kwenye viwanja vilivyokuwa na  nyasi bandia hivyo hicho nacho ndio kitu ambacho kilipelekea wao kushindwa kuchukua pointi tatu muhimu.

    "Tunashukuru walau tumepata pointi moja lakini timu yangu
haikucheza vema kutokana na kuzoea kucheza kwenye nyasi bandia hivyo tutajitahidi kuhakikisha tunapata pointi tatu kwenye kila mechi ya Ligi kuu "Alisema Kibadeni.

Alisema ligi kuu soka Tanzania bara mzunguko wa pili ni ngumu kwa kusema matarajio yake ni kuhakikisha wanafanya vziuri kwenye mechi zao zinazofuata kwani hicho ndio kitu pekee ambacho kitampa ridhaa ya wao kuendelea kubaki kwenye mashindano hayo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »