TWFA KUSAKA WAFADHILI KWA AJILI YA LIGI YA WANAWAKE.

March 10, 2014
CHAMA cha Mpira wa Miguu wa wanawake nchini Tanzania (TWFA)kimesema kuwa  kipo kwenye mikakati kabambe ya kutafuta wafadhili ambao wataweza kusaidia kufadhili ligi  za wanawake kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini ili kuweza kuinua kiwango cha soka hilo.

Katibu wa Chama hicho Taifa,Amina Karuma aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi mkoani hapa ambapo alisema mikakati hiyo ni pamoja na kushirikisha na shirikisho la soka nchini TFF ili kuweza kuendeleza mpira wa miguu kwa wanawake kupitia programu ya grass root inayoshirikisha wanawake na wanaume.



Karuma alisema mpango wa mafunzo ya grass root utawawezesha vijana kuendeleza na kukuza vipaji vya soka hapa nchini na hatimaye kuweza kuinua kiwango cha soka kitendo ambacho kitasaidia kupatikana wachezaji wazuri ambao watailetea mafanikio timu zetu za Taifa.

      "Sasa hivi chama kipo kwenye mkakati kabambe kuhakikisha
tunachezesha ligi ya soka kwa wanawake nchini nzima na hilo
litafanyika kwa kushirikiana wafadhili ambao watapatikana "Alisema Karuma.

Hata hivyo alisema wataweka utaratibu mzuri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuweza kuwekeza soka la wanawake hapa nchini na hatimaye kupatikana timu nzuri za Taifa za wanawake ambazo zitalileta heshima nchi yetu.

Alisema mpira wa wanawake una changamoto nyingi tofauti na ilivyo michezo mwengine hapa nchini hivyo watashirikiana na shirikisho la soka hapa nchini kuhakikisha wanapata wafadhili ili kuweza kuchezesha ligi za woka kwa wanawake kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »