SERIKALI kupitia
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum
imeendelea kuimarisha huduma za malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto
katika ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika, zikiwemo jitihada
mbalimbali za kuhamasisha na kufanya ushawishi kwa watoa maamuzi na
watunga Sera ili masuala ya malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto yapewe
kipaumbele.
Ameyasema hayo Machi 11, 2024 Jijini Dar es salaam
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dorothy
Gwajima wakati akisoma hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano wa kimataifa wa
malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kwa nchi za ukanda wa
Afrika Mashariki kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“imewezesha
nchi nyingi Barani Afrika kuwa na Sera na Programu maalum za masuala ya
malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto na Serikali za nchi
mbalimbali zimeweza kufanya maamuzi ya kutoa elimu bure katika shule za
msingi pamoja na kuanzisha na kuyafanya madarasa ya awali kuwa sehemu ya
elimu ya msingi”.
Aidha, baadhi ya nchi za Afrika zimeandaa na
zinatekeleza Sera maalum kwa ajili ya Watoto, Mwaka 2016 Jumuiya ya Nchi
za Afrika Mashariki iliandaa Sera ya Mtoto inayotekelezwa kwa pamoja na
nchi za Afrika Mashariki ambayo pamoja na mambo mengine inaelekeza
kuimarishwa kwa huduma za malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.
Pia
Hali hiyo imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za malezi, makuzi na
maendeleo ya awali ya mtoto hasa wale wanaoishi katika maeneo ambayo
hakuna huduma ya vituo vya kulelea watoto wadogo mchana haipatikani.
Aidha,
malezi na makuzi ya watoto kwa sasa yanaathiriwa na changamoto
mbalimbali zikiwemo migogoro ya familia ambayo waathirika wakubwa ni
watoto, Wazazi au Walezi hawana muda wa kulea watoto wao kwa kuwa busy
zaidi na shughuli nyingine na kuacha watoto wanajilea au kulelewa na
watu wengine, tunahitaji kutafakari na kuchukua hatua ili kuepukana na
baadhi ya vikwazo katika malezi ya watoto wetu.
“tunapaswa
kulijadili ni ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano ambao una
manufaa mengi lakini pia umekuja na changamoto zake kwa watoto na wazazi
au walezi ambapo, watoto wanahusishwa na matumizi yasiyofaa ya mitandao
(online platforms) yanayopelekea watoto kufanyiwa ukatili mitandaoni
(Online Child Explaitation and Abuse)”.
Hivyo, nasisitiza mila
nzuri kwani nyingine zina madhara kwa watoto, Mfano wa Mila yenye
madhara kwa watoto ni ukeketaji (Female Genitor Mutilation – FGM),
hatupendi kuona watoto wetu wanafanyiwa vitendo hivyo ambavyo vina
madhara kwao.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Anna Athanas Paul
amesema Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa
mtu mzima. Mwana mpumbavu ni mzigo kwa mamaye lakini mwana mwenye hekima
ni fahari kwa babaye. Kwa hiyo wamama ni jukumu letu kuleta wana wenye
hekima
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert
Chalamila amesema kila mtoto ametokana na mzazi ambaye ni Baba na Mama
na mtoto huyo anaweza kuwa na mlezi ambaye ni ndugu wa wazazi, kutokana
na ukweli huo hakuna jambo linalosababisha kuwepo kwa watoto wanaoitwa
wa mtaani kwani hakuna mtaa unaozaa watoto.
TANGA RAHA BLOG
habari
SERIKALI IMEENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA MALEZI, MAKUZI NA MAENDELEO YA MTOTO UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon