TANZANIA YAPIGA HATUA KUBWA KUTOKOMEZA MATENDE NA MABUSHA

March 12, 2024

Na Sophia Kingimali

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema nchi imepiga hatua kubwa katika kuhakikisha inatokomeza magonjwa ya matende na Busha kwa kuokoa watu milioni 31.2 waliokuwa na hatari ya kupata maambukizi ya vimelea vya ugonjwa huo.

Alizungumza na waandishi wa Habari leo Machi 12,2024 jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa kuhusu hatua zilizofikiwa katika kutokimeza ugonjwa huo nchini hususani mkoa wa Dar es salaam.

Amesema awali maambumizi makubwa ya ugonjwa huo yalikuwa katika Halmashauri 119 ambapo serikali kwa kushirikiana na wadau wameza kudhibiti ugonjwa huo katika Halmashauri 112 kati 119 na kubakiwa na Halmashauri 7.


Amesema katika mkoa wa Dar es salaam Halmashauri zote yaani ya manispaa ya Kigamboni na Ubungo,Temeke na Halmashauri ya jiji hazina maambukizi mapya ya ugonjwa huo baada ya kusitisha umezeshaji wa kingatiba na kubaki na kata 10 za Halmashauri ya Kinondoni ambazo zinamaambukiza mapya kwa asilimia 2.3.

“Kutokana na matokeo haya wizara ya Afya inapenda kutoa taarifa rsmi kwa wananchi wa mkoa huu tunasitisha kampeni za uwezeshaji wa kingatiba ya ugonjwa lakini pia nitoe rai kwa wananchi kuchukua taadhari kwa kufanya usafi na kuua mazakia wa mbu”,!amesema Ummy.

Amesema zoezi la umezeshaji kingatiba utafanywa kwa kata 10 za manispaa ya Kinondoni ambazo ni Tandale,Kijitonyama,Mwananyamala,Kigogo,Mzimuni,Magomeni,Ndugumbi,Hananasif,Kinondoni na Makumbusho.

Aidha Waziri Ummy ametoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo kujitokeza kwa wingi kushiriki kampeni hiyo ya kingatiba zitakazoendelea kufanyika kwenye maeneo yao ili kuweza kutokomeza maambukizi ya ugonjwa huo.

Sambamba na hayo Waziri Ummy amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuunga mkono jitihada za kutokomeza magonjwa yaliyokuwa ayapewi kipaumbele.

“Kupitia mkutano wa ‘Reaching the last mile’uliofanyika mwezi Desemba 2023 huko Dubai Rais aliahidi kuwekeza kiasi cha dola za kimarekani milioni tatu karika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2024 ili kufanikisha kutokomeza magonjwa haya hususani Matende na Mabusha.”amesema.

Akitaja Halmashauri zenye maambukizi mapya hivi sasa ni Pangani,Mafia,Kinondoni,Kilwa,Lindi Manispaa,Mtama na Mtwara Mikinfani ambako kuna jumla ya wakazi 1,203,359.    

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »