ALIYEMUUA MTOTO WAKE WA MIAKA MITATU MBARONI

January 24, 2024

 


Na. Abel Paul,Jeshi la Polisi- Arusha.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linamshikilia mtu mmoja aitwaye Amedius Mfoi (25) dereva bodaboda mkazi wa Muriet Jijini Arusha kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake aitwaye Amani Amedius Mfoi (03) Mkazi wa Morombo jijini Arusha.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishna msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Januari 23,2024 muda wa saa 12:00 jioni mtaa wa Murieti Tarafa ya Elerai katika manisipaa ya jiji la Arusha.

Kamanda Masejo amebainisha kuwa mtuhumiwa huyo alimkata shingo mtoto huyo na kitu chenye ncha kali na kutenganisha kichwa na kiwiliwili.

Aidha ameeleza kuwa baada ya taarifa hizo kufika Jeshi la Polisi mara moja Jeshi hilo lilianza uchunguzi na kumtafuta mthumiwa huyo kwa kushirikiana na wananchi ambapo walifanikiwa kumkamata muda mchache baadae.

ACP Masejo amesema baada ya uchunguzi Jalada litapelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »