Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amefika katika Ofisi ya Halmashauri ya Jiji la Arusha kuona utekelezaji wa Agizo la Chama Cha Mapinduzi aliilotoa la kumtaka Mkuu wa Mkoa kuhakikisha Ofisi inafunguliwa na kusikiliza, kutatua na kusuluhisha migogoro, kero na changamoto mbalimbali za Wananchi.
Makonda amesema jambo hilo lisiwe la siku moja na isiwe kusubiria hadi viongozi wa kitaifa waje na watoa maagizo na badala yake wao wenyewe kujiwekea taratibu hizo ili kusudi kuhakikisha changamoto za Watanzania zinatatuliwa kwa wakati na kufikia dhamira ya Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
EmoticonEmoticon