BODI YA WADHAMINI HOSPITALI YA MUHIMBILI YAZINDUA KAMATI MBILI, YAJIWEKEA MIKAKATI YA MIAKA MITANO

March 15, 2018


Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini (MNH), Dkt. Ellen Mkondya-Senkoro wakati akizindua Kamati mbili ya Kudhibiti Uadilifu na Uratibu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (katikati) akitambulisha viongozi na wajumbe wa Kamati mbili ya Kudhibiti Uadilifu na Uratibu.

Viongozi wa kamati ya Kamati mbili ya Kudhibiti Uadilifu na Uratibu wakijitambulisha.
Viongozi wakifuatilia uzinduzi huo.
Kiongozi kutoka idara ya utawala bora, ofisi ya Rais, Ikulu kwa kushirikiana na taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakitoa mafunzo elekezi na wawezeshaji kwa kamati zilizochaguliwa.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Ellen Mkondya-Senkoro (wa tatu toka kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wajumbe wa kamati mbili zilizochaguliwa.
Picha/Habari: Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.


BODI ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Menejimenti yake imejiwekea mikakati mbalimbali katika mpango mkakati wake wa miaka mitano kuanzia mwaka 2017 hadi mwaka 2022 unaolenga kuimarisha utawala bora ambao ni muhimu katika utekelezaji wa mikakakati mingine inayolenga kuboresha huduma kwa wagonjwa.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Ellen Mkondya-Senkoro wakati akizindua Kamati mbili ya Kudhibiti Uadilifu na Uratibu.

Amesema pamoja na ueledi wa kazi, uadilifu katika utumishi wa umma ni pamoja na kutokuomba rushwa au kutoa rushwa wakati watumishi wa umma wanapotekeleza majukumu yao. "Hospitali ya Taifa Muhimbili inau
nga mkono mkakati wa Taifa dhidi ya rushwa na mpango mkakati wa utekelezaji wa awamu ya tatu (2017-2022).

"Nina imani kwamba kamati hizi zitatekeleza majukumu yake ipasavyo kuhakikisha kwamba mkakati huu unatekelezwa kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali," amesema Dk. Mkondya-Senkoro.

Ameongeza utawala bora ni pamoja na kuwepo kwa uadilifu wa hali ya juu katika taasisi ambao kawaida unasimamiwa na Bodi ya wadhamini na pia kuzingatiwa kwa ukaribu na viongozi watendaji na watumishi katika taasisi husika.

"Kwa mantiki hiyo, bodi ya wadhamini na Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na menejimenti yetu tumejiwekea mikakakati yetu ya miaka mitano na lengo kuu ni kuhakikisha tunaboresha huduma kwa wateja wetu ambao ni wagonjwa," amesema.

Amefafanua kamati ambazo wamezizindua leo ni kwamba ya kamati ya kwanza itakuwa ya uratibu ambayo itakuwa kamati ya uongozi itakayosimamia utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kudhibiti uadilifu katika hospitali hiyo.

Amesema kamati ya pili ni kamati ya kudhibiti uadilifu ambayo ndio itahusika na utekelezaji na mikakati ya kudhibiti uadilifu na kuziwasilisha taarifa zake katika kamati ya uongozi kwa hatua zaidi.

"Niwaambie kwamba wajumbe kamati hizi mbili wamepewa mafunzo elekezi na wawezeshaji kutoka idara ya utawala bora, ofisi ya Rais, Ikulu kwa kushirikiana na taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

"Nina imani kubwa baada ya ya mafunzo kamati zitaweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo kama yalivyoanishwa kwenye mkakati wa Taifa dhidi ya rushwa na mpango wa utekelezaji wa awamu ya tatu," amesema.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »