Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amekagua maendeleo ya mradi wa
upanuzi wa miundombinu ya kituo cha afya Songwa pamoja zahanati ya
Maganzo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Katika
ziara hiyo Telack alikagua ujenzi wa chumba cha upasuaji na maabara
katika kituo hicho cha afya ambayo unaotekelezwa kwa fedha zilizotolewa
na Benki ya Dunia (WB) sh. milioni 400.
Akiwa
Songwa aliwapongeza wananchi kwa akujitolea katika shughuli za
maendeleo umoja na kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha wanapata
maendeleo katika maeneo yao ikiwa ni kuboresha huduma.
“Niwapongeza
wananchi kwa kujitolea kushiriki shughuli za ujenzi na tumekuja hapa
tumeona mmejitokeza kwa wingi kujenga kituo chenu siku. Siku zote umoja
ni nguvu na utengano ni udhaifu kazi itakwenda haraka na kwa muda mfupi
kwa sababu ninyi mmeamua kusema kile kitu ni cha kwenu,” alisema.
Mhe.
Telack aliwataka wananchi kuwapa ushirikiano watumishi wa afya ambao
wanawahudumia na kutoa taarifa kwa viongozi wao endapo wanaona
wanakwenda kinyume cha taratibu za kazi.
Pia
aliwataka watumishi wasivunjike moyo kutokana na baadhi ya changamoto
zinazojitokeza pindi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao huku
akiwaahidi kuwa Serikali iko nao bega kwa bega.
Awali
akiwasilisha taarifa ya Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga
Taraba alisema huduma ya upasuaji katika kituo hicho cha afya itaanza
baada kukamilika kwa majengo ya upasuaji.
Alisema
Halmashauri kwa kushirikiana na wananchi, Serikali Kuu na wadau
mbalimbali wa maendeleo wanaendelea kujenga vituo vya afya na zahanati
kwa kutenga fedha kwa ajili ya ukamilishaji.
Mhe.
Taraba aliongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri imetenga
jumla ya sh. 100,000,000 kwa ajili ya kukamilisha jengo la afya ya
baba, mama na mtoto katika hospitali ya wilaya.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na watumishi pamoja na
wananchi katika viwanja vya kituo cha afya cha Songwa alipofanya ziara
kukagua mradi wa afya. Wengine pichani kulia ni Mkuu wa Wilaya ya
Kishapu, Nyabaganga Taraba na diwani wa kata ya Songwa, Abdul Ngoromole.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na wananchi
wanaojitolea nguvu kazi akiwa katika mradi wa upanuzi wa kituo cha afya
Songwa wilayani Kishapu.
Sehemu
ya watumishi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack
(hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao viwanja vya kituo cha afya
Songwa.
Mganga
mfawidhi wa zahanati ya Maganzo, Sam Phillip akitoa maelezo kuhusu
kituo hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack
alipokitembelea.
Wananchi wa kata ya Songwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack viwanja vya kituo cha afya Songwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na watumishi pamoja na
wananchi katika viwanja vya kituo cha afya cha Songwa alipofanya ziara
kukagua mradi wa afya.
Mkuu
wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akitoa taarifa ya wilaya kwa
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na ujumbe kutoka mkoani
alipowasili ofisini kwake tayari kwa kuanza ziara.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya, Peter Mwita akitoa maelezo kuhusu shughuli za afya katika zahanati ya Maganzo.