Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda akikabidhi Msaada wa Vitanda 4o na Magodoro 40 kwa Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe kwaajili
ya hospitali ya mwananyamala jijini Dar es Salaam ikiwa ni kusheherekea
siku ya Mwanamke duniani ambayo hufanyika kila mwaka Machi 8. Benki hii
imetoa vitanda na magodoro kwaajili ya wodi ya akina mama katika
hospitali hiyo.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe akimpongeza Mkuu wa Matawi
ya Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda kwa msaada waliotoa benki ya
Exim vitanda 40 na Magodoro 40 kwaajili ya wodi ya akinamama
wanaojifungua.Ikiwa ni Kusheherekea siku ya mwanamke ambayo hufanyika
Machi nane kila Mwaka.
Mlezi
mkuu (Patroni) wa hospitali ya Mwananyamala, Musa Wambura
(aliyesimama)akizungumza katika hafla fupi ya benki ya Exim kukabidhi
vitanda 40 na magodoro 40 katika hospitali ya Mwanayamala jijini Dar es
Salaam leo kwaajili ya wodi ya akinamama wanaojifungua.
Mkuu
wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda akizungumza kabla ya
kukabidhi msaada wa vitanda 40 na magodoro 40 katika hospitali ya
Mwananyamarla jijini Dar es Salaam leo.Katikati ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe na kushoto ni Mkuu waMatawi ya Kanda Getrude Mbunda.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe akishukuru kwa Mkuu
wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda kwa kuiona
hospitali ya Mwananyamala kwa kuwa kunahospitali nyingi"Tunashukuru
Mchango wenu sana Mungu awabariki ."
kushoto ni Mkuu waMatawi ya Kanda Getrude Mbunda na Kulia ni Mkuu wa matawi ya Kanda Elizabeth Mayengo.
BENKI YA EXIM TANZANIA NA KAMPENI YAKE YA MWAKA MZIMA YA KUSAIDIA JAMII.
BENKI ya
Exim Tanzania leo imekabidhi vitanda na magodoro 40 kwa Hospitali ya
rufaa Mwananyamala, jijini Dar es Salaamkwa kuwa Benki ya Exim Tanzania
iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka jana, kwa
kuzindua mradi wa mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujali jamii” ambao
Benki hiyo itawekeza katika sekta ya afya Tanzania hasa kwenye kuboresha
huduma za afya zinazotolewa kwa wakina mama na wanawake.
Makabidhiano
hayo yamefanyika katika hospitali ya Mwananyamala wakiongozwa na
wafanyakazi wanawake wa Benki ya Exim kwenye hospitali hiyo jengo la
utawala katika hospitali hiyo ukipokelewa na Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mwananyamala Dk. Khadija Shebe.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Mkuu wa Matawi ya benki ya Exim, Agnes Kaganda
amesema “Katika kuadhimisha sherehe za wanawake mwezi huu, Benki ya Exim
inatambua mchango wa wanawake katika kujenga jamii na kwenye ukuaji wa
uchumi. Msingi wa mpango wetu huu wa mwaka mzima wa kujali jamii ni
kuelewa kiasi gani wanawake ni muhimu katika jamii".
Benki
imejitolea kusherehekea maadhimisho ya miaka 20 kwa kusaidia wanawake
kwa kuboresha huduma za uzazi katika sekta ya afya. Tunaamini kwamba
tuna sehemu kubwa ya kufanya mabadiliko mazuri katika sekta mbalimbali
katika jamii zetu na sisi tumejizatiti kwenye mpango huu."
Kaimu
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija
Shebe alipongeza Exim Bank Tanzania kwa msaada wake na kuhimiza taasisi
mbalimbali kutekeleza ishara ya Benki ya Exim Tanzania katika kusaidia
kuboresha huduma ya afya kwa wanawake nchini. Aliongezea kwa kusema
“Upungufu wa vitanda katika mahospitali ni changamoto kubwa. Msaada huu
kutoka benki ya Exim wa hivi vitanda 40 na magodoro utasaidia sana
katika kupunguza changamoto hii .”