Katika Picha Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina na ujumbe wake akiwa akiwa katika
ziara katika kituo cha Taifa cha uzalishaji Mbegu bora za Mifugo kwa
njia ya chupa, (NAIC) kilichopo Mjini Arusha.
Katikati Katibu Mkuu
Mifugo Dkt. Maria Mashingo akisoma Hotuba katika zoezi la uzinduzi wa
madume ya kisasa ya mbegu bora za Ng’ombe katika kituo cha taifa cha
uzalishaji mbegu bora kilichopo mjini Arusha, Kushoto ni waziri wa Mfugo
na Uvuvu Mhe. Luhaga Mpina, na kulia ni Mkurugenzi wa Uzalishaji Mifugo
na Masoko wa Wizara hiyo, Dkt.Lowlence Asiimwe.
Katikati Waziri wa Mifugo
na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiangalia dume bora la kisasa kutoka nchi
ya New Zealand katika kituo cha Taifa cha Uhimilishaji cha (NAIC) Arusha
jana alipokuwa katika ziara maalum ya uzinduzi wa Madume hayo.kulia
ni Dkt Paul Mollel, Mkurugenzi wa Kituo hicho.
NA,
MWANDISHI MAALUM - ARUMERU
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imepewa wiki mbili kufanya tathmini kuona
kama kuna haja ya kuagiza maziwa na mazao yake kutoka nje ya nchi na
kama waagizaji wanafuata taratibu na masharti ya kisheria yaliyowekwa
na Serikali.
Hayo yameelezwa jana
na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina alipokuwa katika ziara
ya kutembelea kituo cha Taifa za uzalishaji wa mbegu Bora za Mifugo
kwa njia ya chupa kilichopo Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.
Waziri Mpina pia aliitaka
Wizara yake kuandaa mpango kazi utakao wezesha kuzalisha Ng’ombe
milioni moja kwa mwaka kuanzia mwaka wa fedha 2018/19 ili kuweza
kusaidia kujenga viwanda vya maziwa na kuweza kumudu soko la ndani
na hata kuhudumia bara zima la Afrika na kusaidia kuongeza pato
la Taifa.
“Kuna makampuni 43
nchini yanayoingiza maziwa toka nje ya nchi,na makampuni 81 yanayojishughulisha
na maziwa na mazao yake,Wizara ifanye tathmini kama kweli tunahitaji
kuingiza maziwa hayo. Alisisitiza Mpina.”
Aliongeza kuwa maziwa
mengi yanaingia ndani ya nchi kwa kupitia njia za panya, na kusema kuwa
wale wote wanaojishughulisha na biashara hizo wapo hatarini kukamatwa
na sheria itachukua mkondo wake. “Mimi na Wizara na yangu tumejipanga
kimwili kiroho na kiakili tutawashughulikia wote wanaofanya biashara
hizi kimagendo hakuna suluhu kwa yeyote atakaye kamwatwa. Alisisitiza.”
Sambamba na hilo, Waziri
Mpina pia alimpongeza katibu Mkuu Mifugo Dkt Maria Mashingo kwa kazi
kubwa ya kuhakikisha kuna kuwepo na mbegu za kutosha kwa kuwepo kwa
madume bora 26 hadi sasa yenye uwezo wa kuzalisha jumla ya dozi 3,120,000
kwa mwaka.
Kwa upande wake, Dkt.
Mashingo alimshukuru Waziri kwa kutoa maelekezo ambayo yanalenga kuleta
mapinduzi ya mifugo na kwamba ameyapokea na yatatekelezwa mara
moja kama alivyoagiza.