Naibu
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameupa Siku 14 Mgodi wa Dhahabu wa Katavi
& Kapufi uliopo Mkoani Katavi kuhakikisha uwe umekamilisha taratibu
za kuajiri Watanzania na kupunguza wafanyakazi wa kigeni kwenye nafasi
ambazo Watanzania wanazimudu kama Sheria inavyoelekeza.
Alitoa
agizo hili jana Tarehe 24 Februari, 2018 alipofanya ziara kwenya mgodi
huo ili kujionea shughuli zinazofanyika katika mgodi huo.
Taarifa
ya mgodi iliyowasilishwa kwake ilibainisha kuwa jumla ya wageni 48
wameajiriwa na huku 36 kati yao wakiwa hawana ujuzi na wanafanya
shughuli ambazo Watanzania wanamudu, ikiwemo ya ulinzi.
Biteko
alisema dhamira ya Serikali ni kuona Watanzania wananufaika na Sekta ya
Madini kwa namna mbalimbali ikiwemo ya kujipatia ajira kwenye migodi na
kwamba suala hilo la kuajiri wageni kwenye nafasi wanazomudu Watanzania
halivumiliki.
Alimuagiza
Mkuu wa Wilaya na Afisa Madini kuhakikisha wanalifuatilia jambo hilo na
liwe limemalizika baada ya wiki mbili kuanzia Tarehe 24 Februari, 2018
na apatiwe mrejesho wake.
“Mnawafanyakazi
wengi ambao wanafanya kazi ambazo Watanzania wanaziweza. Hatuwabagui
lakini tunataka manufaa ya madini yabaki kwa Watanzania,” alisema
Biteko.
Biteko
aliiagiza Idara ya Uhamiaji Nchini kufuatilia Wafanyakazi wakigeni
waliopo migodini ili kukagua kama wanavyo vibali vya kufanya kazi hapa
nchini. “Mnavyotoa vibali muwe makini, ili shughuli zinazokuja kufanywa
na wageni ziwe kweli Watanzania hawazimudu,” alisisitiza.
Alihimiza
migodi yote nchini kuepuka kuwanyanyasa wafanyakazi sambamba na
kuwataka wafanyakazi waliaoajiriwa migodini kufanya kazi kwa uaminifu
ili kulijengea Taifa heshima inayokubalika.
aibu
Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa
Wilaya ya Mpanda, Lilian Matinga (katikati) wakati wa kukagua shughuli
ziazofanyika kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Katavi & Kapufi Ltd uliopo
Mkoani Katavi.
Naibu
Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa pili kulia) akitembelea maeneo
mbalimbali ya Mgodi wa Dhahabu wa Katavi & Kapufi Ltd uliopo Mkoani
Katavi ili kujionea shughuli zinazoendelea mgodini hapo. Wa pili kulia
ni Mbia na Makamu Mwenyekiti wa Mgodi wa Katavi & Kapufi Ltd,
Sebastian Kapufi
Moja ya eneo la mitambo kwenye mgodi wa Dhahabu wa Katavi & Kapufi Ltd uliopo Mkoani Katavi