Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Daudi Yassin akiwa na viongozi wa chama hicho wakikabidhi msaada waliupeleka wakati wa kutimiza miaka 41 ya chama cha mapinduzi
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Daudi Yassin akiwa na viongozi wa chama hicho wakikabidhi msaada waliupeleka wakati wa kutimiza miaka 41 ya chama cha mapinduzi huku wakiwa wameonyesha moja ya msada walioupeleka kwa watoto yatima na hayo ni maziwa yanayozalishwa na kampuni ya Asas
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Daudi Yassin akiwa na viongozi wa chama hicho wakikabidhi msaada waliupeleka wakati wa kutimiza miaka 41 ya chama cha mapinduzi huku wakiwa wameonyesha moja ya msada walioupeleka kwa watoto yatima na hayo ni maziwa yanayozalishwa na kampuni ya Asas
Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi wakiwa wamebeba misaada waliyokuwa wanaipeleka kwenye vituo vya watoto yatima
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Daudi Yassin akiwa na viongozi wa chama hicho wakikabidhi msaada waliupeleka wakati wa kutimiza miaka 41 ya chama cha mapinduzi
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Daudi Yassin akiwa na viongozi wa chama hicho wakikabidhi msaada waliupeleka wakati wa kutimiza miaka 41 ya chama cha mapinduzi wakiwa na mmoja ya viongozi wa kituo cha watoto yatima wa kituoa cha Makalala
NA FREDY MGUNDA,MUFINDI.
CHAMA cha mapinduzi wilaya ya
Mufindi kimesherekea miaka 41 ya chama hicho kwa kufanya kazi za kijamii kwa
kwenda kuwatembea watoto yatima wa vituo viwili vilivyopo katika halmashauri ya
Mji wa Mafinda kwa kusikiliza kero zao na kutoa msaada wa vitu mbalimbali.
Akizungumza wakati wa kukabidhi
msaada kwenye kituo cha makao ya watoto Lutheran kinachomilikiwa na kanisa la
KKT na kituo cha makao ya watoto Makalala kinachomikiwa na kanisa la kikatoriki
ambavyo vyote vipo katika halmasahuri ya
Mji wa Mafinga,mwenyekiti wa chama hicho, Daudi Yasini alisema kuwa chama cha
mapinduzi kinasherekea miaka 41 kwa kufanya kazi za kijamii kama alivyoagiza
mwenyekiti wa chama hicho taifa.
“Mwaka huu imekuwa tofauti na
miaka ya nyuma safari hii ni kufanya kazi kwa kuwatumikia wananchi hivyo
tunapaswa kufanya kazi kwa vitendo hivyo naombeni wananchi na viongozi kufanya
kazi kwa kujituma na kuhakikisha tunatimiza malengo ya ilani yetu” alisema
Yassin
Yassin alisema kuwa wameamua
kutembelea vituo vya watoto yatima kwa lengo la kuitaka jamii kwa ujumla kuwa
kumbuka watoto hao ambao wanamahitaji mengi huku wakikumbana na changamoto
nyingi za kimaisha katika vituo wanavyoishi.
“Mmejione wenyewe kuwa hawa
watoto wanaishi kwa kutegemea misaada hivyo tunapaswa kuijenga jamii kwa kujitolea
misaada mbalimbali kwa kuwasaidia watoto yatima na wale wanaishi katika
mazingira magumu” alisema Yassin
Aidha Yassin alisema kuwa chama
cha mapinduzi kinachukizwa na vitendo vya kikatili kwa watoto akina mama hata
akina baba hivyo ni lazima jamii ikomeshe vitendo vyote vya ukali wa kijinsia
ili kuwa na jamii inatazama maendeleo.
“Jamani hakuna kitu ambacho
chama chetu hatupendi kama kusikia maswala ya ukatili wa kijinsia tunaomba
jamii ibadilike mara moja na kuwa jamii inayoogopa na kupinga ukatili wa
kijinsia,niwaombe watanzania kwa ujumla tukatea ukatili wa kijinsia” alisema Yassin
Kwa upende wake katibu wa chama
cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Elirehema Nassar alisema kuwa wametoa
msaada unaogharimu zaidi ya shilingi milioni moja kwa ajili ya kuwajali
wananchi na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
“Sisi lengo letu ni kuhakikisha
wananchi wanaishi katika mazuri na kukifurahili chama chetu,tumeleta hii
misaada ambayo inatasaidia kwa kiasi furani kuwapa faraja watoto na viongozi wa
vituo hivi ambavyo tumevitembelea hii leo” alisema Nassar
Nassar alisema kuwa chama hicho
haitawavumia viongozi na watu ambao watakwamisha juhudi za Rais John Pombe
Magufuli za kuwaletea maendeleo watanzania.
“Nitapambana nao kwa kasi zangu
zote na nguvu zote kwa wale ambao watakuwa wanaleta mambo ya ajabu katika jamii
kwa kujifanya yeye anajua kuliko viongozi wa serikalia au anapinga kila kitu
kinachofanywa na Rais wetu” alisema Nassar
Philipo Kamoga na Helena Msefe Walikipongeza
chama cha mapinduzi kwa kutimiza miaka 41 kwa kufanya kazi za kijamii ambazo
zinasaidia kutatua changamoto ambazo zinawakabili wananchi wa kipato cha chini.
“Kwanza tunaopenga kwa dhati
kwauwa chama cha kwa hapa nchi kufikisha miaka 41 ambayo haijafikiwa na chama
chochote kile hapa nchini hongereni sana” walisema viongozi hao