Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa kwanza
) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga
( wa tatu ) wakiruka viunzi wakati walipotembelea jana ili
kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi katika eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ambao umeombwa na uongozi wa mkoa wa Iringa
kufutwa ili kujenga mji mpya wa kitalii katika mkoa huo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah akizungumza
na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu ambao alikutana nao kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa
huo katika kikao cha tatu cha kamati hiyo kilichofanyika jana
mkoani Iringa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa pili kulia) Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) wakiwa wameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (katikati) wakipatiwa maelezo na Mkuu wa Idara ya mipango miji wa Halmashauri
ya Iringa, Wilberd Mtongani ( wa tatu kushoto) wakati walipotembelea eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi ya kuhaulisha eneo hilo. Wengine ni Watalaamu
ni wataalamu kutoka ofisi ya Mkoa pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa tatu kulia) Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet
Hasunga ( wa pili kushoto) wakiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa
ya Ushauri wa Misitu, Prof. Shabani Chamshama (wa kwanza kushoto) wakipatiwa maelezo na
Afisa mipango miji wa Halmashauri ya Iringa, Wicliph Benda ( wa tatu kushoto) wakati walipotembelea
eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ili kujiridhisha kabla ya
kutoa maamuzi ya kuhaulisha eneo hilo. Wengine ni Watalaamu ni
wataalamu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Naibu Waziri wa Wizara Japhet Hasunga ( wa kwanza ) akiwa ameambtana na wataalam
kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa wakiruka viunzi wakati
alipotembelea jana ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi katika
eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ambao umeombwa na uongozi wa mkoa wa Iringa kufutwa ili kujenga
mji mpya wa kitalii katika mkoa huo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa pili
kushoto) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga
( wa tatu kushoto) wakioneshwa ramani ya eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa
Kilolo na Mkuu wa Idara ya mipango miji wa Halmashauri ya Iringa
Wilberd Mtongani ( wa kwanza kulia) wakati walipotembelea eneo hilo kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi ya kuhaulisha ili kujenga mji mpya wa kitalii mkoani Iringa
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa kwanza
kulia ) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki
Dkt. Ezekiel Mwakalukwa ( katika ) wakati walipotembelea jana eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi wa eneo hilo ambalo limeombwa na uongozi wa mkoa wa Iringa kuhaulishwa ili kujenga
mji mpya wa kitalii katika mkoa huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah, Naibu Waziri
wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza
wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri
wa Misitu ambapo Waziri Kigwangallah anakutana nao kwa mara ya kwanza
tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo katika kikao cha tatu kilichofanyika jana mkoani Iringa.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu wakimsikiliza
Waziri Kigwangallah katika kikao cha tatu kilichofanyika jana mkoani
Iringa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu, Prof. Shabani Chamshama akitoa neno la shukrani kwa viongozi
kwa niaba ya Wajumbe wa kamati hiyo katika kikao cha tatu kilichofanyika
jana mkoani Iringa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa kwanza
kulia ) akiwa ameambatana na wataalam wakati alipotembelea jana eneo la msitu wa
hifadhi wa Kihesa Kilolo ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi
wa eneo hilo ambalo limeombwa na uongozi wa mkoa wa Iringa kuhaulishwa
ili kujenga mji mpya wa kitalii katika mkoa huo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza ( wa pili kushoto) akiwa ameambatana na baadhi ya waandishi wa habari pamoja na wataalamu kutoka mkoani wakitembea kuangalia mipaka ya eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa
Kilolo ambao umeombwa na uongozi wa mkoa huo kufutwa ili kujenga mji mpya wa kitalii katika eneo hilo.
(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT)
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangallah
amesema kuwa hatajibu maombi yoyote yaliyowasilishwa ofisini kwake kutoka
kwa Wakuu wa mikoa, Halmashauri pamoja na Wakuu wa wilaya ya kufuta
maeneo ya Hifadhi ili maeneo hayo yaweze kutumika Kwa ajili ya
matumizi mengine.
Amesema kuwa maeneo hayo yalitengwa kisheria na yana
umuhimu mkubwa kiuchumi na kijamii hivyo lazima yaendelee kuhifadhiwa
kwa ajili ya faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Amesema katika kipindi cha Uwaziri wake hatajibu ombi
lolote lile linalohusu kubadili matumizi ya maeneo hayo kwa vile kuwa
na misitu sehemu za mijini ni sehemu ya maendeleo.
Aliyasema hayo jana mjini Iringa wakati alipokuwa
akizungumza kwa mara ya kwanza na kamati ya kitaifa ya ushauri wa misitu
iliyokutana kwa ajili ya kufanya kikao chake cha tatu tangu ilipoundwa
mwaka jana ikiwa pamoja na kutembelea msitu wa Hifadhi wa kihesa Kilolo
uliiombwa na uongozi wa mkoa kufutwa ili upate kutumika kwa kuweka miundo
mbinu mipya ya mji wa kitalii.
Katika kikao hicho ambacho Mkuu wa mkoa wa Iringa,
Amina Masenza alishiriki, Waziri Kigwangallah alimuomba Mkuu huyo
awafikishe ujumbe Wakuu wa mikoa wengine ambao walituma na wanaotarajia
kutuma maombi ya namna hiyo kuwa yeye hatakaa ayajibu hadi pale tu yule
aliyemteua ampe maelekezo na si vinginevyo"
Amesema kuwa Halmashauri nyingi nchini kila zikiona
maeneo ya Hifadhi zimekuwa zikifikiria kubadili matumizi ya maeneo
hayo ili yatumike kwa shughuli zingine za maendeleo kama vile kupima
viwanja ili kuwauzia wananchi kwa lengo la kukusanya mapato.
"Ofisin kwangu kuna maombi mengi mno ambayo hata sielewi nianze na lipi
na niache lipi, nasema sitajibu ombi lolote lile" alisisitiza Waziri
Kigwangallah.
Aidha, Waziri Kigwangallah mara
baada ya kuzungumza na kamati hiyo alitembelea eneo la hifadhi ya msitu
huo huku akiwa ameongoza na kamati hiyo pamoja na Uongozi wa
Mkoa wa huo .
Katika kutembelea eneo hilo, Waziri Kigwagwallah aliwashukia
viongozi wa Halmashauri kwa kuanzisha dampo katika
eneo hilo huku kamati ikijionea magari matatu ya taka yakiendelea
kumwaga uchafu kwenye eneo hilo jambo ambalo ni kinyume na sheria za
uhifadhi.
Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga aliwashukia
watendaji wa mkoa huo wakati walipokuwa wakipishana kutoa
maelezo kuhusiana na mipaka na matumizi ya eneo hilo endapo Wizara
itaridhia ombi lao la kubadili matumizi ya eneo hilo.
Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alimuhakikishia
Waziri kuwa eneo hilo endapo watapewa litatumika kwa malengo yaliyokusudiwa
na si vinginevyo.
Waziri Kigwangallah mara baada ya kutembelea eneo
hilo wakati akitoa majumuisho yake, Alisema kuwa kufuatia ziara hiyo
anasubili ushauri utakaotolewa na kamati ya kitaifa ya msitu ndipo atakapokuwa
na jibu kuhusiana na ombi la kubadilia matumizi la eneo
hilo .
Pia, Waziri Kigwangallah aliiagiza ofisi ya Mkuu
wa Mkoa kuhakikisha kuwa maeneo ya milima kwa vile sio moja ya
maeneo ya hifadhi yaongezwe katika eneo la hilo lengo likiwa
ni kuzuia uharibifu wa uoto wa asili unaoendelea katika maeneo hayo.
Awali, Mwenyekiti wa Kamati hiyo wakati akitoa neno la shukrani
alimhakikishia Waziri kuwa watamshauri jambo lolote lile linalohusu
misitu bila kujali litamfurahisha au litamuudhi, kitakachoangaliwa hapo
ni maslahi mapana ya taifa.
Katika hatua nyingine ,Waziri Kigwangallah ameitaka Wakala wa
Huduma za Misitu nchini (TFS) kuanza kuweka nguvu nyingi katika kuhifadhi
misitu baadala ya kuvuna na kufanya biashara ya mazao ya misitu.
Alisema licha ya kuwa TFS imekuwa ikifanya vizuri
katika baadhi ya maeneo lakini katika suala la kuhifadhi misitu imekuwa
kama vile sio kazi yake " yenyewe kazi yake
imekuwa ni kuvuna kilichopandwa, kuuza na kukusanya mapato yatokanayo
na mazao ya misitu" alisema.
Wakati huo huo, Waziri Kigwangallah amesema Wizara
inakusudia kuchukua misitu yote iliyo chini ya vijiji na Halmashauri
kwa vile zimeshindwa kuisimamia ipasavyo na hivyo kupelekea sehemu kubwa
ya nchi kugeuka kuwa jangwa.
Mbali na hilo amewaonya wananchi wanaowazuia watendaji
kuweka vigingi katika mipaka ya hifadhi, huku wengine wamekuwa wakivingoa
na wengine kuhamisha vigingi hivyo kutoka eneo moja hadi jingine kuwa
waache tabia hiyo moja la sivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa
dhidi yao. .