Wanahabari Hellena Mwango, Careen , Kulwa Mwaibale na mke wa Patrick Mwillongo wakiwa wamekaa nje ya jengo la Hospitali ya Mkoa Temeke wakitafakari namna ya kumsaidia Mwillongo walipofika kumjulia hali leo hii asubuhi.
Na Mwandishi Wetu
Ndugu wanahabari mwenzetu Patrick Mwillongo yupo hoi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ambako amelazwa kwa matibabu.
Mwillongo anasumbuliwa na ugonjwa wa kujaa maji kwenye mapafu ambao umesababisha hashindwe kujimudu kufanya jambo lolote.
Kwa umoja wetu na tabia tuliojijengea kama wanahabari tujitokeze kumsaidia mwenzetu ambaye anapita katika kipindi kigumu.
Mwillongo ni Mwandishi wa Habari wa kujitegemea
na anafanya shughuli zake wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na awali alikuwa akiandikia magazeti mbalimbali likiwemo Jambo Leo na yale yanayomilikiwa na Kampuni ya New Habari.
Kwa atakayegusa kumsaidia anaweza kutoa mchango wake kupitia namba MPESA-0754362990, Tigo Pesa ni 0712727062