Baadhi ya wananchi wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa zana haramu za uvuvi kwenye Kijiji cha Nkome Wilayani Geita . |
Wananchi wa Kata ya Nkome wakiwa kwenye mkutano ambao ulikuwa na lengo la kuelezea hali ya uvuvi haramu ilivyo kwenye kata ya Nkome na namna ambavyo oparesheni imeweza kufanyika kwenye maeneo hayo. |
Kiongozi wa kikosi maalumu kinachoendesha oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu ziwa victoria Gabriel Mageni akielezea namna ambavyo wameweza kuendesha zoezi hilo ndani ya siku kumi na mbili. |
Mkuu
wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisisita kwa wale ambao ni
watumishi na viongozi kuacha kuendelea na tabia ya kushirikiana na
wavuvi haramu .
Na,Joel Maduka,Geita.
|
Serikali
Mkoani Geita Imeteketeza zana haramu zenye thamani ya shilingi milioni
therathini na tatu zikiwemo Nyavu za makila zilizounganishwa
2,393,makokolo ya sangara 32,timba 142 makokoro ya dagaa 7 na dududu 11.
Hatua
hiyo imetokana na oparesheni ya Kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu
ambayo inaendelea kwenye maeneo ya ziwa viktoria ikiwa na lengo la
kuondoa uvuvi huo ndani ya ziwa hilo pamoja na kuondoa mitandao ya
wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia ,biashara ya samaki wachanga
na utoroshaji wa samaki na mazao ya yake,kwenda nje ya nchi kinyume cha
sheria.
Zoezi
hili la uteketezaji zana hizo limefanyika kwenye Kata ya Nkome ,ambapo
kiongozi wa oparesheni hiyo Gabriel Mageni ,amemweleza mkuu wa mkoa
huo kwamba kuna baadhi ya wafanyakazi wa hifadhi ya Rubondo wamekuwa
wakihusika na uvuvi haramu kwa kuwaruhusu wavuvi kuingia kwenye hifadhi
na wengine kuficha zana zao ndani ya hifadhi na kwamba wamekuwa
wakilipwa fedha wafanyakazi hao maarufu kwa jina la “KIFUNDA”
Kufuatianmalalamiko
hayo mtandao huu umetafuta kwa njia ya simu afisa mahusiano wa TANAPA
Pascal Shelutete alisema kuwa wao kama watu ambao wanamamlaka ya hifadhi
za taifa na kwamba kwa mujibu wa kanuni na taratibu za sheria askari
wao hawapaswi kushiriki kwenye vitendo vya ujangili na kwamba taratibu
za kiuchunguzi zikifanyika na wakabaini kuna watumishi wanajihusisha na
vitendo hivyo hatua za kisheria na za kinidhamu zitachukuliwa na
hawawezi kuwakingia kifua.
Aidha
Mageni aliongeza kuwa katika operesheni hiyo ambayo ina siku kumi na
mbili baadhi ya mambo ambayo wameyabaini ni pamoja na baadhi ya
viongozi wa vijiji na maofisa wanaosimamia maeneo ya uvuvi kuwapa
hifadhi raia wa kigeni wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi wakiwa
hawana kibali na kusababisha serikali kukosa
mapato.
mapato.
Mkuu
wa Mkoa huo,Mhandisi Robert Luhumbi,amewataadhalisha watendaji ambao
wanashirikiana na wavuvi haramu na kwamba endapo kuna mtu hakibainika na
kitendo hicho serikali itahakikisha inamchukulia hatua na kwamba
kupitia oparesheni hiyo hatabakia hata mtu mmoja ambaye anajihusisha na
shughuli hizo.
Nyawalwa
Wange ni moja kati ya watu ambao wanajishughulisha na kazi ya uvuvi
alisema agizo la Mkuu wa Mkoa ni la kuungwa mkono kutokana na kwamba
uvuvi haramu umeendelea kuharibu kwa kiasi kikubwa samaki
ambao wapo ndani ya ziwa viktoria na kwamba serikali iendelee kuwabaini wale wote ambao wanaendelea kufanya shughuli za uvuvi kinyume na sheria.
ambao wapo ndani ya ziwa viktoria na kwamba serikali iendelee kuwabaini wale wote ambao wanaendelea kufanya shughuli za uvuvi kinyume na sheria.
Katika oparesheni hiyo jumla ya fedha ambazo zimekusanywa ni zaidi ya milion, 111 fedha
zinazotokana na faini ,malipo ya mrahaba pamoja na mauzo ya samaki.
zinazotokana na faini ,malipo ya mrahaba pamoja na mauzo ya samaki.