Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
mkewe Mary wakizungumza na Mama Maria Nyerere wakati walipomtembelea
nyumbani kwake Mwitongo, Butiama Januari 20, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
mkewe Mary wakiongozana na Mama Maria Nyerere kuingia kwenye uwanja wa
Mwenge katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu katika
kijiji cha Butiama Januari 20, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mama Maria Nyerere wakati alipomtembelea nyumbani kwake
Mwitongo, Butiama Januari 20, 2018. Kulia ni mkewe Mary .
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary
Majaliwa akiwasha mshumaa kwenye kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Nyerere eneo la Mwitongo, Butiama, Januari 2018. Wapili kushoto ni Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na kushoto ni mkewe Naima .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
mkewe Mary wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Nyerere eneo la Mwitongo, Butiama Januari 20, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ,
Mkewe Mary na Mama Maria Nyerere wakiwapungia wananchi katika mkutano
wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika uwanja wa
Mwenge kijijini Butiama Januari 20, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mwenge katika kijiji cha Butiama Januari 20, 2017
Wananchi wa Butiama
wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano
wa hadhara kwenye uwanja wa Mwenge katika kijijini hapo Januari 2018
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary
Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Butiama katika mkutano wa
hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa
Mwengekijijini hapo Januari 20, 2018.
Mama Maria Nyerere akiwasalimia
wananchi wa Butiama katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Mwenge kijijini hapo Januari
20, 2018.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu