Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.
Tanzania
inataraji kuwa wenyeji wa mkutano mkubwa wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Duniani FIFA (Fifa Summit) utakaofanyika February 22, 2018 kwenye
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Mkutano huo mkubwa wa pili unaofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania unashirikisha nchi 19 Wanachama wa Fifa.
Mkutano huo utakaoongozwa na Rais wa FIFA Gian Infantino pia
utahudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF) Ahmad
Ahmad,Makamu wa Rais wa Fifa,Katibu mkuu wa Fifa na viongozi mbalimbali
wa FIFA na CAF ikiwemo wajumbe wa kamati ya utendaji.
Wageni kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano huo wataanza kuwasili Tanzania Februari 20, 2018
Ajenda za mkutano huo mkubwa wa Fifa ni miradi mbalimbali ya Fifa
zamani ikifahamika kama Goal Project na sasa ikifahamika Fifa Forward
Programme,ajenda ya soka la vijana,Wanawake na klabu wakati ajenda
nyingine ya mkutano huo ni kujadili kalenda ya kimataifa ya
Fifa,kuboresha masuala ya uhamisho na vipaumbele vyake
Nchi zitakazoshiriki ni Bahrain,Palestina,Saudi Arabia,Umoja wa Falme za Kiarabu(UAE),Algeria,Burundi, Africa ya Kati,Ivory Coast,Mali,Morocco,Niger, Tunisia,Bermuda,Monserrat,St, Lucia,Us Virgin,Maldives,Congo na wenyeji Tanzania.
Akizungumzia Mkutano huo unaofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania
Rais wa TFF Ndugu Wallace Karia alisema TFF inajivunia kupata uwenyeji
huo mkubwa wa mkutano wa FIFA na hiyo inachangiwa na mahusiano mazuri na
wadau mbalimbali ambayo yamezaa matunda.
Rais Karia ameongeza kuwa hiyo ni fursa kubwa kwa Serikali kupitia
Wizara zake kuweza kutumia fursa hiyo ambayo inaweza kusaidia katika
upande wa Uchumi.