DK. KIGWANGALLA NA MKURUGENZI MKAZI WA UNDP KUANZISHA KIKOSI KAZI CHA KUCHUNGUZA TUHUMA ZA UJANGILI WA TEMBO KATIKA HIFADHI YA RUAHA

January 02, 2018
Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam
.....................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY wamekubaliana kuanzisha kikosi kazi cha pamoja cha kuchunguza tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na kituo cha habari cha ITV LONDON kuhusu ujangili wa Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyopo Mkoani Iringa.

Dk. Kigwangalla na Mkurugenzi huyo, wamefikia makubaliano hayo leo Januari 2, 2018 wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Waziri Kigwangalla amemueleza Mkurugenzi huyo kuwa Wizara yake inaandaa mikakati mbalimbali ya kuongeza idadi ya watalii nchini na mapato ikiwemo kuwashirikisha wananchi kuandaa mwezi maalum wa Urithi wa Tanzania pamoja na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato kwa njia za kielektroniki katika vituo mbalimbali ya Utalii.

Kwa upande wake, Mkurugenzi huyo amemuahidi Waziri Kigwangalla kuendelea kumpa ushirikiano katika nyanja mbalimbali za kuendeleza Utalii nchini na uhifadhi wa misitu na wanyamapori kwa ujumla.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo, Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo, Mpingo House Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akiagana  na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP), Bi. Natalie BOUCLY baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo, Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »