Mfanyabiashara, Emmanuel Mallya (kushoto) akimkabidhi hati na mkataba wa zahanati EB Zahanati Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Michael Kilawila kwenye hafla hiyo ya makabidhiano. |
Makabidhiano ya hati na mkataba wa zahanati EB yakifanyika katika hafla hiyo. |
Makabidhiano ya hati na mkataba wa zahanati EB yakifanyika katika hafla hiyo. |
Na Mwandishi Wetu, Moshi
MFANYABIASHARA na
mzaliwa wa Kijiji cha Uchau Kaskazini wilaya ya Moshi Vijijini,
Emmanuel Mallya, ameikabidhi serikali zahanati ikiwa na vifaa vya kisasa
vikiwamo vitanda vya wagonjwa vinavyotumia nishati ya umeme.
Zahanati
hiyo inayojukana kwa jina la EB zahanati, imejengwa na mfanyabiashara
huyo kwa kutumia nguvu zake mwenyewe bila kuhusisha msaada kutoka
Halmashauri ya wilaya ya Moshi wala serikali kuu.
Akizungumza
katika hafla fupi ya kuikabidhi zahanati hiyo kwa serikali,
mfanyabiashara huyo alisema wazo la kujenga zahanati hiyo lilitokana na
kuwepo na changamoto za umbali wa huduma za afya kwa wananchi wa eneo
hilo.
Alisema
changamoto hiyo ilipelekea kuwepo na vifo vya watu wengi
vilivyochangiwa na umbali wa upatikanaji wa vituo vya afya na kwamba
changamoto hizo ndizo zilizomsukama kuona haja ya kujenga zahanati hiyo.
Alitoa
wito kwa mamlaka husika kuitunza zahanati hiyo pamoja na vifaa
vitakavyotumika katika kuwahudumia wagonjwa huku akitoa wito kwa watu
wengine wenye uwezo kujitolea katika kuwahudumia wananchi wasio nacho.
“Utajiri
unatokana na moyo wa mtu alionao, unaweza ukawa na utajiri na usiwe na
moyo wa kuwasaidia wengine, kila mtu amepewa karama na mwenyezi Mungu,
muhimu hapa ni namna ya kuzitambua hizo karama,” alisema.
Kabla
ya ujenzi huo ulioanza julai mwaka 2013, familia iliyokuwa ikishi
mahali ilipojengwa shule hiyo iliridhia ombo la mfanyabaishara huyo la
kuachia eneo hilo na kupelekwa kwenye eneo jingine kwa ushirikiano wa
Chama cha Msingi cha Ushirika cha Kimasio.
Aliwapongeza
familia hiyo kwa kukubali ombi lake la kuliachia eneo hilo na kuongeza
kuwa, bila familia hiyo kuridhia kuondoka katika eneo hilo ndoto zake za
kujenga zahanati katika eneo hilo zingeishia ukingoni.
Mbunge
wa Jimbo la Moshi Vijijini, Anthony Komu alihimiza usimamizi wa karibu
wa zahanati hiyo kwa wale watakakuwa wasimamizi baada ya aliyeijenga
kuikabidhi kwa serikali.
"Mhehsimiwa
Mkuu wa Wilaya, uzoefu unaonyesha kuwa, miradi mingi inayojengwa na
wafadhili imekuwa ikiharibika kutokana na kutokuwepo na usimamizi wa
karibu, ni rai yangu kuwa tuitunze zahanati hii isijekuwa mazalia ya
popo kama ambavyo tumekuwa tukishuhudia kwa baadhi ya zahanati na vituo
vya afya,” alisema.
Alisema
mfanyabiashara huyo ametenda wema wa hali ya juu kwa wananchi wa Wilaya
ya Moshi Vijijini na Vunjo kwa ujumla na kwamba wema huo kamwe
hautafutika ndnai ya mioyo ya wananchi hao.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Michael
Kilawila, alitoa wito kwa wananchi wa wilaya hiyo kuchangishana kwa kile
kidogo walichonacho ili wanunue gari la wagonjwa ambalo litahudumia
zahanati hiyo kwa muda wa saa 24.
Alisema
uwepo wa gari la wagonjwa katika zahanati hiyo utarahisisha kuwapeleka
wagonjwa katika Hospitali kubwa ikiwamo ya Kibosho, Mawenzi na KCMC kwa
wale ambao watahitaji kupewa rufaa.
Alisema
maendeleo yanahitaji umoja na mshikamano na kuonya kuwa maendeleo
hayana itikadi yoyote ya kisiasa kwani zahanati hiyo itahudumia wananchi
wote bila kujali huyu ni wa chama gani.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Mkuu wa wilaya ya Moshi, Kippi Warioba alipongeza
moyo ulioonyeshwa na mfanyabiashara huyo wa kusaidia watu wenye
mahitaji. Pia alitoa wito kwa serikali ya kijiji hicho kuanza mazungumzo
na wananchi wanaoishi karibu na zahanati hiyo kuachia maeneo yao ili
zahanati hiyo ipanuliwe na kufika hadhi ya kituo cha Afya.
Alitoa
wito kwa kila mtu kuchangia chochote alichonacho ndani ya jamii na si
lazima iwe pesa na kuwapongeza walioachia eneo ilipojengwa zahanati hiyo
wametoa mchango mkubwa sana kwa jamii.
______________________________ ______________________________ _______________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mobile:- 0717
030066 / 0756 469470