WAFANYABIASHARA WA WANYAMAPORI HAI NJE YA NCHI WAIOMBA SERIKALI IWASAIDIE

January 10, 2018
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia)    akifungua kikao cha  Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai   kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara, kushoto ni  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Nebbo Mwina ( Picha na Lusungu Helela-MNRT)
 Mwenyekiti wa Chama cha wasafirishaji  wanyamapori hai nje ya nchi, Enock Balilemwa  akizungumza kwenye kikao cha cha Wizara ya Maliasili na Utalii na Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara. ( Picha na Lusungu Helela-MNRT)
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Nebbo Mwina   akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kufungua kikao  cha  Wawakilishi wa Wafanyabiashara  ya Wanyamapori hai kilichofanyika jana  mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara. ( Picha na Lusungu Helela-MNRT)
 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wasafirishaji  wanyamapori hai nje ya nchi, Fatuma Hamisi akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (hayupo pichani)    kwenye kikao cha cha Wizara ya Maliasili na Utalii na Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai kilichofanyika jana mjini Dodoma ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara. ( Picha na Lusungu Helela-MNRT
 Baadhi ya Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati wa kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma kati ya Wizara na wadau hao lengo  likiwa ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara. ( Picha na Lusungu Helela-MNRT)
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga na Wawakilishi wa Wafanyabiashara  ya Wanyamapori hai kwenye kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni kuiomba Wizara kusitisha zuio la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara. ( Picha na Lusungu Helela-MNRT
Mjumbe wa Halmashauri wa TWEA, Paul Madinda ambaye pia ni mmiliki wa shamba la viumbe hai jijini Arusha, akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (hayupo pichani) jinsi alivyoathirika tangu zuio hilo la kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi lilipotelewa   kwenye kikao cha cha Wizara ya Maliasili na Utalii na Wawakilishi wa Wafanyabiashara ya Wanyamapori hai kilichofanyika jana mjini Dodoma. ( Picha na Lusungu Helela-MNRT
Chama cha wasafirishaji  wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara (TWEA)   kimeiomba serikali isitishe zuio la kusafirisha nje wanyamapori hao ili wanachama wake  waweze kujikwamua na hali ngumu ya maisha inayaowakabili.
Wakizungumza mbele ya  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga   kwenye kikao  cha Wizara na wawakilishi wa  Wafanyabiashara hao waliiomba serikali isikilize kilio chao.
Kwa upande wake , Mwenyekiti wa Chama hicho, Enock Balilemwa alisema baadhi ya wanachama wakiwemo walemavu waliokuwa wamechukua mikopo   benki wamefukuzwa kwenye nyumba zao baada ya kushindwa kufanya marejesho ya mikopo hiyo kufuatia zuio la biashara hiyo.
Alieleza kuwa baadhi ya wanachama wake wamejikuta kwenye hali ngumu ya kupoteza mali zao na kuingia kwenye mifarakano na wateja wao kwa vile  wafanyabiashara hao walichukua pesa toka kwa wateja kama  malipo ya awali hivyo wakati wa zoezi la kusimamisha biashara linafanyika liliwakuta wafanyabiashara hao wameshachukua pesa za wateja wao kama malipo ya awali.
Naye, Makamu Mwenyekiti wa TWEA, Fatuma Hamis alimweleza Naibu Waziri kuwa  zuio hilo lilifanywa ghafla mno bila kutoa muda kwa wafanyabiashara hao ukizingatia kuwa walikuwa wakimiliki leseni halali walizokuwa wamezilipia pesa bila kuzifanyia kazi ya kuwaingizia kipato.
Aidha, alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa zuio hilo limepelekea wafanyabiashara hao kupoteza uaminifu kwa wateja wao na kuwaweka kwenye mazingira magumu ya ushindani kibishara kwani biashara hiyo haifanywi na Tanzania pekee.
Wakati akijibu hoja za Wafanyabiashara hao,  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewahakikishia  Chama cha wasafirishaji  wanyamapori hai nje ya nchi kibiashara (TWEA) ,kuyafanyia kazi malalamiko yao kadri itakavyowezekana na kuja na kauli moja ya serikali.
Amesema lengo la serikali la kuzuia usafirishaji wanyamapori hao lilikuja baada ya wafanyabishara ambao sio waaminifu kukengeuka kwa kuanza kujihusisha na ujangili pamoja na kusafirisha wanyamapori ambao hawamo kwenye orodha ya vibali walivyopewa.
‘’Dhumuni la serikali la kusitisha biashara hii  ilikuwa ni njema tu baada ya kuona wajanja wachache wananufaika huku wanyonge wakibaki watazamaji kwenye rasilimali zao’’ alisema Hasunga
Hata hivyo, Naibu Waziri Hasunga alisema lengo la serikali halikulenga kuwakomoa bali ni kutaka kuweka mfumo mzuri utakaomsaidia kila  Mtanzania aone ananufaika na rasilimali za nchi yake.
‘’Nimewasikiliza kwa umakini wa hali ya juu lakini hata hivyo Serikali ina utaratibu wake wa kutoa majibu, tupeni muda ili tukitoa majibu kuhusu hoja zenu kuwe na jibu moja kwa kila mmoja wetu’’ alisema
Katika hatua nyingine, Hasunga aliwataka wafanyabishara hao wasisite kuonana nae  muda wowote ule  kwa kumpigia simu au kwa kuonana nae pindi wanapokuwa na jambo la kutaka kuzungumza nae kwa ajili ya manufaa mapana ya Wizara na nchi kwa ujumla.
Naye, Kaimu Mkurugenzi  wa Idara ya wanyamapori, Dkt. Nebbo Mwina aliwahakikishia wafanyabiashara kufanyia kazi malalamiko yao kutokana na   hoja za msingi  zilizowasilishwa na wafanyabiashara hao.
‘’Nimesikia baadhi ya malalamiko yenu ambayo kwa nafasi yangu niliyo nayo kwa kushirikiana na watumishi walio chini yangu nitayashughulikia’’ alisema.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »