MAKAMU WA RAIS AZINDUA BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR

January 10, 2018

8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni tayari wa Uzinduzi wa Baraza la Vijana Zanzibar akiongozana na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mhe. Maudline Cyrus Castico pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Ndugu Khamis Rashid Kheri
15
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mhe. Maudline Cyrus Castico wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza la Vijana Zanzibar
22
Sehemu ya waliohudhuria uzinduzi wa baraza la vijana Zanzibar.
26
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihamasisha vijana wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Vijana Zanzibar akiwa pamoja  na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mhe. Maudline Cyrus Castico na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Ndugu
Khamis Rashid Kheri.
35
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Vijana uliofanyika kwenye ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani, Kikwajuni.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa jamii haina budi kutambua kuwa vijana wana fursa kubwa katika kuleta maendeleo ya nchi .
Makamu wa Rais aliyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Vijana Zanzibar uliofanyika kwenye ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Kikwajuni.
Makamu wa Rais alisema kuwa Baraza la Vijana Zanzibar ni Chombo au jukwaa litakalowavusha vijana kufikia maendeleo wanayohitaji kiuchumi, kijamii, kisiasa na kufuatana na kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia Duniani.
“Ni imani yangu kuwa Baraza hili litakuza mioyo yenu ili muweze kujituma, kujiendeleza na kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono serikali yenu pamoja na kutetea na kuyalinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kuenzi fikra za Muasisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume (Mungu amrehemu)”
Makamu wa Rais aliendelea kusema kuwa Uzinduzi wa Baraza la Vijana Zanzibar ni mwendelezo wa mawazo ya Wana Mapinduzi ya kutaka kuweka hali za wananchi kuwa sawa (Bora), na kujenga Taifa lenye Vijana Imara.
Makamu wa Rais alisisitiza kuwa ni matarajio yake kuwa Baraza la Vijana Zanzibar litaendeshwa kwa misingi ya demokrasia na sheria, kanuni na miongozo ya taasisi itakavyoelekeza.
Baraza hilo linalotokana na Sera ya Maendeleo ya Vijana ya Mwaka 2005, sera hii ndio iliyopelekea kupitishwa kwa sheria nambari 16/2016 iliyoanzisha Baraza hilo, hatua ya utekelezaji wa Mkataba wa Vijana Afrika 2006 ambapo Jamhuri ya Muungano imeridhia.
Makamu wa Rais aliwataka Vijana kuwa mstari wa mbele katika kutunza amani ya nchi, kutoa ushauri pale wakiwa na mawazo mbadala, kutengeneza mtandao na kuitumia mitandao kwa manufaa ya kuwaleta pamoja na kukemea vitendo vyote vya udhalilishwaji wa watoto na wanawake.
Mwisho; Makamu wa Rais aliwataka vijana hao kuwa wamoja na kujenga hali ya kujitegemea na badala kuwa tegemezi, watetezi wan chi, kuibua mawazo mapya ya maendeleo na washiriki kwa kupaza sauti katika mambo yanayowahusu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »