Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein katika
sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika
uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani humo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi
wengine wa kitaifa wakiwa wamesimama wakati gwaride la
heshma(halionekani pichani) lilipokuwa likipita katika sherehe za miaka
54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani
Karume kisiwani humo.
Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali
Mohamed Shein akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria katika sherehe
za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa
Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.
Rais mstaafu wa awamu ya Tatu
Benjamini Mkapa akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na Rais
mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume katika sherehe za miaka 54 ya
Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume
kisiwani Zanzibar.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akipokea Saluti kutoka kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo
pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro mara baada ya
kuhudhuria sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika
katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani Zanzibar.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na wanachi mara baada ya sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya
Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Abeid Amani Karume kisiwani
Zanzibar.
Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akipungia mkono wakati akiwasili katika uwanja wa Amani.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa
cha Zanzibar SUZA wakipita mbele ya jukwaa kuu katika maandamano ya
sherehe za sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili katika uwanja
wa Amani kisiwani Zanzibar.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiondoka katika uwanja wa Amani mara baada ya kuhudhuria sherehe za
miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi
pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara
baada ya kuwasili katika uwanja wa Amani kwa ajili ya kuhudhuria sherehe
za sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali
Mohamed Shein akikagua gwaride la Heshma katika sherehe za miaka 54 ya
Mapinduzi ya Zanzibar zolizofanyika katika uwanja wa Amani.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya
sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zolizofanyika katika uwanja
wa Amani.
PICHA NA IKULU