Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akizungumza na Rais wa Shirikisho la
viwanda vya misitu Tanzania (SHIVIMITA) Ben Sulus (kulia) wakati Rais
huyo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya wamiliki wa viwanda vya
mazao ya misitu wakati wa kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma,
ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa Wizara kukutana
na wadau wa Wizara kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto
zinazowakabili. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki,
Dkt. Ezekiel Mwakalukwa
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na
wawakilishi wa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu mara baada
kufungua kikao kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la
kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa Wizara kukutana na wadau wa
Wizara kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili.
Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel
Mwakalukwa
Rais wa Shirikisho la viwanda vya
misitu Tanzania (SHIVIMITA) Ben Sulus akiwasilisha taarifa ya
wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu kwa Naibu Waziri wa Maliasili
na Utalii, Japhet Hasunga wakati wa kikao kilichofanyika jana mjini
Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi wa Wizara
kukutana na wadau wa Wizara kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto
zinazowakabili.
Baadhi ya wawakilishi wa wamiliki
wa viwanda vya mazao ya misitu wakimsikiliza Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii , Japhet Hasunga kwenye kikao kilichofanyika
jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni muendelezo wa viongozi
wa Wizara kukutana na wadau wa Wizara kuwasikiliza na kuzifanyia kazi
changamoto zinazowakabili
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akizungumza kabla ya
kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga
kufungua kikao cha wawakilishi wa wamiliki wa viwanda vya mazao ya
misitu kilichofanyika jana mjini Dodoma, ikiwa lengo la kikao hicho ni
muendelezo wa viongozi wa Wizara kukutana na wadau wa Wizara
kuwasikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili.
Picha na Lusungu Helela-MNRT
………………..
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga amewahakikishia wamiliki wa viwanda vya mazao ya
misitu nchini kuwapa ushirikiano wa kutosha pale inapohitajika kwa
kuzishughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kwenda
sambamba na azma ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda.
Amesema Wizara ya Maliasili na
Utalii imedhamiria kutatua changamoto zinazowakabili ili kuwawezesha
wamiliki wa viwanda hivyo hasa wazawa kutoa ajira nyingi kwa
wananchi.
Amesema Wizara hiyo haiwezi
kufanya kazi pekee yake pasipo kushirikiana na sekta binafsi kwani
wao ndo wamiliki wa viwanda vinavyotoa ajira kwa wananchi ambao ndio
walinzi wakubwa misitu nchini.
Akizungumza kwenye kikao
kilichofanyika jana mjini Dodoma, kati ya viongozi wa Wakala wa Huduma
za Misitu Tanzania (TFS) na Wawakilishi wa Wamiliki wa Viwanda vya
mazao ya misitu nchini, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet
Hasunga aliwataka wadau hao wasisite kuwasiliana nae pale wanapokuwa na
jambo lolote linalohusu maendeleo ya viwanda vyao
‘’Nimechaguliwa na Mhe. Rais kuja
katika Wizara hii kwa ajili ya kufanya kazi nanyi, tufanye kazi kwa
ushirikiano’’ alisema Hasunga
Aidha, Naibu Waziri huyo,
amelisema Serikali imeanzisha utaratibu wa ugawaji wa vitalu kwa njia
mnada na kwa njia ya makubaliano binafsi lengo lake sio kuviua
viwanda wa mazao ya misitu vya vinavyomilikiwa wazawa bali ni kutaka
kila mwenye sifa asiweze kukosa mgao huo.
Akifafanua kuhusiana na utaratibu
huo mpya wa ugawaji wa vitalu ulioanza mwaka jana , Hasunga alisema
asilimi 30 ya vitalu imekuwa ikifanyika kwa njia ya mnada na asilimi
70 imekuwa ikifanyika kwa njia ya makubaliano binafsi hali iliyopelekea
kupunguza malalamiko na pamoja na vitendo vya rushwa kwa wadau.
‘’Kila mmoja wetu hapa atakuwa
shahidi hakuna hata mmoja mwenye kiwanda cha mazao ya misitu aliyekosa
mgao kupitia huu utaratibu mpya ulianza kutumika mwaka jana’’
Alisema kuwa licha ya kuwepo kwa
malalamiko kutoka kwa wamiliki wa viwanda vya mazao ya misitu juu ya
utaratibu huo mpya ambao wengi ni wazawa kwa kushindwa kushindana na
matajiri lakini hata hivyo utaratibu huo kwa njia ya mnada
umeisaidia serikali k kupanga bei stahiki ya soko katika njia ya
makubaliano binafsi.
Hasunga alisema Serikali ipo
tayari kupokea mawazo mapya kutoka kwa wamiliki wa viwanda hivyo kama
wataona kuna umuhimu wa kuboresha utaratibu huo mpya wa ugawaji wa
vitalu.
Wakati akijibu hoja za wadau hao,
Hasunga aliwaagiza waandae ripoti itayoonesha changamoto zinazowakabili
na kuiwasilisha ofisini kwake ifikapo tarehe 10 mwezi ujao kwa ajili ya
kufanyiwa kazi
Pia, Aliwaagiza wamiliki wa
viwandao hao kuunda kitengo kitakachokuwa na jukumu la kufanya tafiti
mbalimbali ikiwemo kujua masoko pamoja na teknolojia rafiki ya
kuzalisha bidhaa zao zitakanazo na mazao ya misitu
Awali, Rais wa Shirikisho la
viwanda vya misitu Tanzania (SHIVIMITA) Ben Sulus wakati akiwasilisha
taarifa yake ameiomba Wizara iangalie namna ya kuwasaidia wamiliki
wazawa viwanda vya mazao ya misitu kwa vile viwanda vilivyo vingi
vimeshindwa kujiendesha kutokana na kukosa malighafi kwa kuwa wazao
hao wameshindwa kushindana na matajiri wakubwa wakati vitalu vinapouzwa
kwa njia ya mnada.
Aliongeza kuwa Wakala wa Huduma za
Misitu (TFS) iangalie uwezekano wa kupunguza bei za vitalu hivyo kwa
kuwa viwanda vingi vimeshindwa kujiendesha kwa vile bei ya soko la mbao
limeporomoka kutokana na watu binafsi kuuza mbao kwa bei nafuu
zilizotokana na miti iliyovunwa ikiwa michanga.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha
Umoja wa Wavunaji Sao Hill, Christian Ahiya, ameiomba Wizara kuona
uwezekano wa kupunguza tozo 32 zinazotozwa kwa wamiliki wa Viwanda vya
mazao ya misitu kwa upande wa wilaya Mufundi kwa kuwa hali hiyo imekuwa
ukiwaumiza na kuwadidimiza.