Mkuu wa Wilaya ya Kishapu,
Nyabaganga Taraba akimtambulisha Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Jumaa Aweso (katikati) kwa wananchi (hawamo pichani), alipofika wilayani
hapo kukagua maendeleo ya huduma ya maji.
Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa amebeba ndoo ya maji na akina mama wa
Kijiji cha Bubiki ikiwa ni ishara ya nia ya Serikali kumuondolea
mwanamke adha ya kero ya maji wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga
alipokuwa akikagua maendeleo ya huduma ya maji.
Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Bubiki,
wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, alipokuwa akikagua maendeleo ya
huduma ya maji.
………………
Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji, Jumaa Aweso ameendelea na ziara yake mkoani Shinyanga kwa
kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa upande wa Sekta
ya Maji katika Wilaya ya Kishapu.
Akihutubia katika mkutano wake kwa
wakazi wa Kishapu, Aweso amewahakikishia wananchi hao kuwa Serikali yao
itafanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha inamaliza kero ya maji
na hakuna kijiji hata kimoja ambacho kitapitwa na huduma ya majisafi.
Naibu Waziri Aweso ametoa rai kwa
wananchi wote kutoa ushirikiano wa dhati kwa Serikali na viongozi wa
ngazi zote, pamoja na kuunga mkono juhudi inazozifanya kwa lengo la
kutimiza upatikanaji wa maji ya uhakika, salama na ya kutosheleza kwa
maendeleo ya Tanzania.
Kwa upande wao wananchi
waliohudhuria mkutano huo wamemshukuru Naibu Waziri wa Maji kwa kazi
kubwa anayoifanya na jinsi anavyojitoa kwa lengo la kuhakikisha kila
mwananchi anafikiwa na huduma ya maji. Pia, wamemtaka afikishe salamu zao za pongezi kwa Rais Magufuli kwa nia yake thabiti ya kuliletea taifa maendeleo.