Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Ndugu
Wallace Karia ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa
CAF kuwa kamishna wa mechi ya kwanza ya ufunguzi wa Fainali za Africa
kwa wachezaji wa ndani CHAN kati ya Morocco na Mauritania itakayochezwa
Januari 13, 2018.
Mchezo huo ambao Rais Karia atausimamia akiwa Kamishna utachezwa kwenye Uwanja wa nyasi asilia wa Mohamed V huko Casablanca.
Waamuzi watakaochezesha mchezo huo ni Janny Sikazwe
kutoka Zambia atakuwa muamuzi wa katikati akisaidiwa na muamuzi msaidizi
namba moja kutoka Kenya Marwa Aden Range na muamuzi msaidizi namba
mbili akitokea Msumbiji Arsenio Chandreque Maringula wakati muamuzi wa
mezani Louis Hakizimana akitokea Rwanda.
Mchezo huo unaohusisha timu mwenyeji unatarajiwa kufuatiliwa na mashabiki wengi zaidi.
Rais Karia hivi karibuni pia aliteuliwa na CAF kuwa
mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya michuano hiyo ya CHAN
itakayoanza Januari 13 mpaka Februari 4, 2018.
Mashindano hayo yanayofanyika kwa mara ya tano(5) bingwa mtetezi akiwa DR Congo.