Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde akizungumza wakati wa
kukabidhi fimbo kwa ajili ya watu wasioona mjini Dodoma,kushoto kwake ni
mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dodoma Neema Majule na kulia kwake ni meneja
wa Next Generation Microfinance Sospeter Kansapa.
Naibu waziri wa nchi ofisi ya
waziri mkuu kazi,vijana na ajira Anthony Mavunde akimkabidhi fimbo
mwenyekiti wa chama cha wasioona mkoa wa Dodoma Omari Lubuva ikiwa ni
msaada uliotolewa na Next Generation Microfinance.
Naibu waziri wa nchi ofisi ya
waziri mkuu kazi,vijana na ajira Anthony Mavunde akiwa na baadhi ya
viongozi wa chama cha wasioona mkoa wa Dodoma na meneja wa Next
Generation Microfinance wakijaribu kutumia fimbo zilizotolewa na taasisi
hiyo kwa ajili ya watu wasioona mkoa wa Dodoma.
Katibu wa chama cha
wasioona(TLB)mkoa wa Dodoma Enock Mbawa akizungumza wakati wa kupokea
msaada wa fimbo kwa ajili ya watu wasioona,kushoto kwake ni meneja wa
Next Generation Microfinance Sospeter Kansapa na kulia kwake ni
mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Dodoma Bill Chidabwa.
Meneja wa Next Generation
Microfinance Sospeter Kansapa akizungumza wakati wa kukabidhi fimbo kwa
ajili ya watu wasioona mkoa wa Dodoma.
Naibu waziri wa nchi ofisi ya
waziri mkuu kazi,vijana na ajira Anthony Mavunde akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa jumuiya za CCM mkoa wa Dodoma na wafanyakazi wa
Next Generation Microfinance baada ya kukabidhi fimbo kwa ajili ya watu
wasioona wa mkoa wa Dodoma.
……………..
NAIBU waziri wa nchi
ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde leo
amekabidhi msaada wa fimbo za kisasa thelathini (30)kwa ajili ya watu
wasioona wa mkoa wa Dodoma huku akitoa rai kwa taasisi binafsi na jamii
kuweka utaratibu wa kusaidia makundi yenye mahitaji.
Msaada huo umetolewa na taasisi inayojishughulisha na kutoa huduma ya mikopo(NEXT GENERATION MICROFINANCE).
Akikabidhi msaada huo
Mavunde ambaye ni mbunge wa Dodoma mjini ameipongeza taasisi hiyo kwa
kutumia faida waliyoipata kusaidia watu wenye mahitaji maalum jambo
ambalo linapaswa kuwa chachu kwa taasisi nyingine pia.
“Ndugu zanguni
mlichokifanya leo kina maana kubwa sio duniani tu bali hata
mbinguni,mmeona ni busara kutumia faida mliyoipata kwa ajili ya kusaidia
wenzetu wenye mahitaji badala ya kutumia kufanya party,naomba utaratibu
huu usiishie leo tu bali muendelee kugusa na makundi mengine yenye
uhitaji,”alisema Mavunde.
Katika kusaidia makundi
hayo ameiomba pia taasisi hiyo kusaidia chama cha waandishi wa habari wa
mkoa wa Dodoma ili waweze kuwa na ofisi yao inayoendana na hadhi ya
makao makuu.
Ametoa rai pia kwa
viongozi wa chama cha wasioona mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanagawa fimbo
hizo kwa walengwa bila ya upendeleo wowote.
Akitoa neno la shukrani
baada ya kupokea msaada huo katibu wa chama cha wasioona(TLB)mkoa wa
Dodoma Enock Mbawa ameishukuru taasisi hiyo kwa kusaidia serikali
kupunguza changamoto walizonazo na kuahidi kuhakikisha fimbo hizo
zinafika kwa walengwa waliokusudiwa.
Awali akimkaribisha
mgeni rasmi meneja wa Next Generation Microfinance Sospeter Kansapa
amesema wameamua kuitikia wito wa rais John Magufuli wa kuwataka wadau
wa maendeleo kote nchini kujitokeza kutoa mchango katika ustawi wa Taifa
wakiamini kuwa fimbo hizo zitakuwa chachu katika kuleta maendeleo ya
Taifa.