Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo akichimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo itakayojengwa eneo la Kijiji cha Lusanga wilayani humo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Like Gugu wakishuhudia tukio hilo
Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu akichimba mtaro kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo eneo la Lusanga wilayani humo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo,Like Gugu
Sehemu ya wananchi wakishiriki katika uchumbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Muheza Mkoani Tanga
Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu akishiriki kubeba tofali kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali itakayojengwa eneo la Kijiji cha Lusanga wilayani Muheza
Sehemu ya wadau wa maendeleo wilayani Muheza wakishiriki kwenye zoezi la ubebaji wa matofali wilayani humo
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa tatu kutoka kulia akiwa na Mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu wa pili kutoka kulia wakipokea mifuko 600 ya saruji kutoka kwa kampuni ya Lucky Cement ya Kisarawe Mkoani Pwani kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu
Sehemu ya shehena ya saruji ambayo ilishushwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kupokea saruji hiyo ambapo aliishurku kampuni hiyo huku akiyataka makampuni mengine yaliyopo mkoani hapa kuunga mkono jitihada hizo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu
Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu akizungumza katika halfa hiyo ambapo aliishukuru kampuni hiyo kwa kuamua kuwasaidia ujenzi huo huku akiyataka makampuni mengine kuiga mfano huo
Meneja Masoko wa Kampuni ya Lucky Cement iliyopo Kisarawe,Emanuel Muya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu azma yao ya kusaidia mifuko ya saruji 600 kwa ajili ya ujenzi wa Hospital ya wilaya ya Muheza kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo,Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu
MKUU wa wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanasha
Tumbo,Mbunge wa Jimbo hilo,Balozi Adadi Rajab na wakazi wa wilaya hiyo wakishirikiana kwa
pamoja wameanza kuchimba msingi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya katika Kijiji cha
Lusanga Kata ya Lusanga ambayo itasaidia kuondoa changamoto ya kutokuwepo kwa
kipindi cha miaka 37.
Hatua ya viongozi hao ina lengo la kuandika historia
tokea wilaya hiyo ilipoanzishwa mwaka 1974 ambapo wananchi walikuwa wakitegemea
kupata huduma za matibabu kwenye hospitali ya Teule Muheza kutoka maeneo
mbalimbali kabla ya kufikiria kuanzishwa kwa hospitali hiyo ambayo
itakayogharimu zaidi ya bilioni 11.
Akizungumza wakati akishiriki zoezi la uchimbaji wa
mtaro wa Hospitali hiyo na kupokea mifuko ya saruji 600 ya Lucky kutoka kwa
Kampuni ya kuzalisha Saruji ya Kisarawe, Mhandisi Mwanasha alisema waliamua
kufanya hivyo kutokana na kuwepo kwa changamoto ya huduma ya afya ambayo
ilimlazimu wakati ameteuliwa kuiongozi wilaya hiyo kukutana na wadau kuweza
kuona namna ya kuweka mikakati ya kupatikana kwake.
Aidha kutokana na kuwepo kwa hospitali ya wilaya
walikuwa wakilazimika kutimia hospitali ya teule Muheza tokea ilipoanzishwa
lakini imeonekana kuzidiwa na watu wanaohitaji huduma hasa ukizingatia pia
zahanati na vituo vya afya vipo vichache huku wananchi wakiongezeka.
“Nilibaini changamoto ya hospitali ya wilaya wakati
nilipokuwa nikifanya vikao kwa kuzunguka kata zote nikaona tatizo la huduma ya
afya ni kubwa sana na hivyo kuonekana kuna haja ya ujenzi wa hospitali ya
wilaya ya Muheza lakini hata kwenye baraza la madiwani suala hilo
lilizungumzwa”Alisema
Mkuu huyo wa wilaya alisema baada ya kufikiria wazo
hilo la ujenzi wa hospitali hiyo waliona wafanya mazungumzo na Agro Tan ambao
wanamiliki Shamba la Muheza Estate ambao walikubali kutoa eneo lao la ekari 100
kwa ajili ya ujenzi huo.
Awali akizungumza katika eneo hilo,Mbunge wa Jimbo
la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu alisema juzi ilikuwa ni siku muhimu sana kwao kutokana na wananchi
kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye msaragambo kwa nia ya kujengwa hospitali
ya wilaya ambacho kilikuwa kilio chao kwa muda mrefu.
Alisema
waliamua kuanzisha mchakato wa ujenzi wa hospitali hiyo baada ya kuona huduma
ambazo zilikuwa zikitolewa katika hospitali ya Teule Muheza kuelemewa kutokana
na watu kuongezeka huku maradhi yakiwa mengi kila wakati na ndio walipoamua
kuchukua uamuzi huo.
Mbunge huyo alisema wananchi wa wilaya hiyo
waliposikia mipango ya kuwepo kwa ujenzi huo walianza kujitolea fedha kiasi cha
elfu mbili ikiwemo kushiriki kwenye uchimbaji wa msingi wa ujenzi wa hospitali
hiyo tokea alfajiri wakiunga mkono juhudi za serikali.
“Lakini pia nisema tunawashukuru kampuni ya Lucky
Cement kwa kutukabidhi mifuko 600 ya saruji na tunategemea pia kuvitumia
viwanda vilivyopo mkoani Tanga kwa lengo la kuongeza nguvu katika ujenzi wa
hospitali ya wilaya yetu tunavifaa vya kutosha vya kuanzia tutaanza na baadae
wataingiza kwenye bajeti kuiomba serikali iwasaidie”Alisema Mbunge huyo
Kwa upande wake,Meneja Masoko wa Kampuni ya Lucky Cement
iliyopo Kisarawe,Emanuel Muya alisema
wao kama wadau wa maendeleo waliguswa na kuamua kuchangia ujenzi wa hospitali
hiyo ili kuwasaidia wananchi kuondokana na changamoto za huduma ya afya katika
wilaya hiyo.
Alisema kwa kutambua thamani ya maendeleo katika
nchi ndio sababu kubwa iliyowasukuma kuamua kusaidia saruji hiyo kwa ajili ya
kuanza mchakato wa ujenzi wa hospitali hiyo ambapo itakapokamilika itawasaidia
kuwaondolea changamoto wananchi.