Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais,TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(katikati) akikagua ujenzi wa
miundombinu ya Afya katika Kituo cha Afya Makole kilichopo katika
Manispaa ya Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais,TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(Kushoto) akimsikiliza Mganga Mfawidhi
wa Kituo cha Afya Makole kuhusiana na maendeleo ya ujenzi wa kituo cha
Afya.
Jengo la Maabara kama linavyoonekana likiwa katika hatua ya Lenta.
Jengo la Wodi ya Kinamama kama linavyoonekana likiwa linefikia katika hatua ya Lenta.
Jengo la Chumba cha Upasuaji kama linavyoonekana likiwa katika hatua ya Lenta.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais,TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa
Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi(katikati) baada ya ukaguzi wa ujenzi
wa miundombinu ya Afya Katika Kituo cha Afya Makole.
Ujenzi wa Chumba cha Kuhifadhia Maiti ukiwa katika hatua ya Lenta.
……………..
Nteghenjwa Hosseah, TAMISEMI.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amevitaka vituo
vyote vya Afya Nchini sambamba na hospital za Wilaya kutengeneza bustani
ya kupumzikia kwa wagonjwa wanaosubiria matibabu katika maeneo hayo.
Waziri jafo ameyasema hayo
wakati akikagua Ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Kituo cha Afya
Makole kilichopo Manispaa ya Dodoma na kuutaka uongozi wa Kituo hicho
kutenegenza bustani ya kisasa pamoja na kupanda miti ya kutosha ili
kutunza matunzingira lakini kupendezesha eneo la hospital.
“Hili Agizo liende kwa Vituo
vyote Nchini pamoja na Hospital za Wilaya zilizoko chini ya TAMISEMI
kuhakikisha wanaekeleza maelekezo haya katika ameneo yote nataka
hospital iwe sehemu ya kupa faraja mgonjwa kwa kupata huduma nzuri
lakini pia kusubiria huduma hiyo katika maeneo yanayovutia wakati wote”
Alisema Waziri Jafo.
Akikagua majengo matano
yanayojengwa katika Kituo hicho cha Afya na kusimamiwa na TAMISEMI
Waziri Jafo amesema ameridhishwa na Ujenzi wa miundombinu hiyo ya Afya
katika Hospital ya Makole kwani umefuata ramani zilizotolewa na Wizara,
unajengwa kwa ubora na uko ndani ya muda wa Utekelezaji.
“Hivi ndio ninavyotaka
wataalamu wangu kujiongeza katika baadhi ya maeneo mfano hapa Mmejenga
Mabara kubwa kulingana na wingi wa wagonjwa mnaowahudumia kwa siku sasa
sio kwa sababu ramani imeonyesha maabara ndogo basi kila mtu anafuata
hivyo hivyo ni lazima tujiongeze kulingana na mahitaji ya ameneo yetu ya
huduma” Alisema Waziri Jafo.
Akizungumzia maendeleo ya
mradi Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makole amesema Ujenzi huu
umesema ujenzi wa Maabara, chumba cha Upasuaji, Wodi ya Kina Mama,
Nyumba ya Mganga pamoja na Ukarabati wa Kichomea Taka utakamilika mapema
mwezi February 2017 na Fedha zilizopokelewa kwa ajili ya ujenzi huo
zitatosha na kukamilisha ujenzi wa miundombinu yote.
Kituo cha Afya Makole ni
miongoni mwa vituo 211 Nchini vilivyopokea/vitakavyopokea Fedha kwa
ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Afya lengo ikiwa ni
kuboresha Miundombinu ya Afya ili kuweza kutoa huduma bora kwa
watanzania.
TAMISEMI YA WANANCHI.