Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Katikati) akikagua mbegu zilizohifadhiwa ghalani kabla ya kuanza kusambazwa alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Wakala wa Mbegu Dkt Sophia Kashenge Kilenge (Kulia) na Meneja uzalishaji Wakala wa Mbegu Ndg Charles Levi (Kushoto). Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Mkurugenzi Wakala wa Mbegu Dkt Sophia Kashenge Kilenge alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo baada ya kukagua baadhi ya mashine za mbegu alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua namna mbegu za mazao mbalimbali zilivyohifadhiwa alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017.
Na Mathias Canal, Morogoro
Naibu Waziri wa Wizara ya
Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa leo Disemba 29, 2017 amewaagiza wafanyabiashara wa
mbolea kote nchini walioweka mgomo wa kupeleka mbolea kwa wakulima kufikia 30
Disemba 2017 wawe wamefungua maghala yao kwa ajili ya kuwauzia mbolea wakulima.
Alisema
endapo wafanyabiashara hao wasipofanya hivyo serikali itawanyang'anya leseni
zao haraka iwezekanavyo ili kuruhusu wafanyabiashara wenye uwezo wa kufanya
jukumu hilo pasina kuwaumiza wakulima kutokana na bei ghali ya mbolea.
Mhe Mwanjelwa ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro
alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) Mara
Baada ya kubaini kuwa kuna wafanyabiashara ambao wameanza kufunga maghala kwa
madai ya kupanda kwa mbolea katika soko la Dunia.
Alisema kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria na kuijaribu
serikali kwani malalamiko yao ya kupanda kwa bei katika soko la Dunia hayana
tija kwani mbolea zote zilipo nchini tayari wakishanunua kipindi soko likiwa
kwenye unafuu mkubwa.
Alisema kuwa serikali ilitoa bei elekezi katika mbolea ya
kukuzia na kupandia ikifahamu fikra kuwa kupitia gharama hiyo wakulima
watanufaika lakini pia wafanyabiashara watanufaika kutokana na faida wanayoipata
lakini wameamua kubadili utaratibu wa kutaka kupata faida kubwa zaidi pasina
kujali wakulima wataumizwa na bei hiyo kwa kiasi gani.
Mhe Mwanjelwa ameitaka kampuni ya Premium ambayo ni moja ya
kampuni zilizogoma kufungua maghala na kupeleka mbolea kwa wakulima kwa bei
elekezi iliyotolewa na serikali.
Alisema kuwa wafanyabiashara hao kwa makusudi wameamua kufifisha
juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ya kuwakomboa wakulima kupitia gharama
nafuu ya mbolea hivyo kufikia kesho wasipofungua maghala hayo watanyang'anywa
leseni zao ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa sheria.