ZAIDI ya
wahamiaji 50 raia kutoka nchini Ethiopia wameka matwa eneo la Duga wilayani
Mkinga mkoani Tanga kwa kosa la kiungia nchini kinyume cha sheria.
Wahamiaji hao wamekamatwa ndani ya kipindi cha mwezi Desemba mwaka huu kutokana na operesheni ambazo
zimekuwa zikiendeshwa na Idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi
ya kuhakikisha wanazibiti wimbi la uingiaji huo.
Hayo
yalisemwa jana na Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Tanga DCI Crispian Ngonyani wakati
akizungumza na gazeti hili ofisi kwake ambapo alisema wahamiaji hao hivi sasa
wanaendelea na kesi zao zinazowakabili kutokana na kuingia nchini kinyume na utaratibu uliopo.
Alisema hatua
ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao inatokana na kuwepo kwa misako ya
kushtukiza katika maeneo mbalimbali hasa ya mipakani mkoani hapa ambapo
wahamiaji hao wamekuwa wakitumia kama njia ya kuingilia.
“Sisi kama
Uhamiaji mkoani Tanga tumejipanga vizuri kuhakikisha wimbi la wahamiaji haramu
hawaingii kutokana na doria ambazo tumekuwa tukizifanya mara kwa mara lakini
kubwa zaidi ni kuwepo kwa vituo eneo la mipakani hususani Horohoro “Alisema.
Aidha
alisema pia ili kuhakikisha suala hilo linazibitiwa kwa vitendo tayari
wamekwisha kuweka kituo eneo la Vijinga wilayani Mkinga kwa kushirikiana na
Jeshi la Polisi wanakagua magari ambayo yamekuwa yakitokea nchini Jirani ya Kenya ili
kuweza kubaini iwapo wahamiaji haramu wamebebwa.
Hata hivyo
alisema kuelekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya wamejiandaa vizuri kuweza
kukabiliana na wimbi la wahamiaji haramu wanaoweza kuingia mkoani hapa kwa
kuendelea operesheni kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo nyumba za kulala wageni
na kwenye hoteli.
“Licha ya
kuendelea na operesheni hizo lakini nisema idadi ya wahamiaji haramu wanaoingia
mkoani Tanga kwa sasa imepungua kwa sababu wakiwakamata wanawapeleka mahakamani pamoja na mawakala wao"Alisem
Afisa Uhamiaji huyo alisema lakini bado tunaendelea kuhakikisha ina koma
kabisa kwa kuwachukulia hatua kali na watanzania ambao watabainika wanashirikiana nao kuwaingia mkoani hapa.