Katibu
Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila( katikati) akielezwa
jambo na Vikosi vya ulinzi na usalama, katika eneo linalotumika kufanyia
mnada wa Madini ya Tanzanite katika eneo la Naisinyai lililoko kwenye
mji mdogo wa Mirerani.
Katibu
Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila( katikati) akiangalia
mapambo na vitu mbalimbali vinavyotengezwa na Kituo cha Uongezaji
thamani Madini ya vito na Miamba( TGC),kilichopo mkoani Arusha, wakati
Mnada wa Madini ya Tanzanite unaofanyika katika Mji mdogo wa Mirerani
mkoani Manyara.
Wanunuzi
kutoka mataifa mbalimbali wakifanya uthamini wa Madini ya Tanzanite
kabla ya mnada kufanyika katika eneo la Naisinyai lililoko kwenye mji
mdogo wa Mirerani.
Vifaa maalum( drum) vilivyohifadhia madini ya Tanzanite.
Madini ya Tanzanite yakipimwa kabla ya kuanza kufanyiwa mnada.
Mjiolojia
Ester Njiwa wa Kituo cha Jemolojia Tanzania( TGC)akionenya vitu
Mbalimbali vinavyotengenezwa na kituo hicho, wakati mnada wa Madini ya
Tanzanite utakaofanyika katika mji mdogo wa Mirerani.
Usajili wa washiriki wa Mnada wa Madini ya Tanzanite ukiendelea katika mji mdogo wa Mirerani mkoani Manyara.
Ukaguzi ukiendelea kwa wanunuzi wanaofika katika eneo linalofanyika mnada wa Madini ya Tanzanite katika Mji mdogo wa Mirerani.
Na Zuena Msuya, Manyara.
Kampuni
tatu za uchimbaji madini ya Tanzanite zimejitokeza kuuza madini hayo
katika mnada wa tatu wa madini ya Tanzanite unaofanyika katika mji mdogo
wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Mshindi wa mnada huo atatangazwa Desemba 21 katika eneo la Naisinyai lililoko kwenye mji mdogo wa Mirerani.
Kamishna
wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka amezitaja kampuni hizo kuwa ni
Tanzaniteone yenye ubia na Shirika la Madini Tanzania( STAMICO),
Tanzanite Afrika na Classic Gems.
Akizungumzia
mnada huo, Kamishna Mchwampaka alisema kuwa utaratibu wa kufanya Mnada
wa Tanzanite ni jitihada za Serikali za kudhibiti utoroshwaji wa madini
hayo nje nchi na pia kuwasaidia wachimbaji na wafanyabiashara wazalendo
kuuza madini yao kwa bei ya ushindani inayoendana na soko la dunia.
Mchwampaka
alifafanua kuwa, mnunuzi atakayefanikiwa kununua madini katika mnada
huo ni yule tu atakayetoa bei ya juu ambayo imefikia au kuvuka bei
inayotokana na Wathamini wa Serikali (Reserve Price).
Aliweka
wazi kuwa zoezi hilo linafanyika kwa njia ya uwazi ambapo wanunuzi wa
ndani na nje wanapata fursa ya kutazama madini na hatimaye kupata nafasi
ya kutayarisha bei zao kwa siri ambazo zitatumbukizwa kwenye sanduku la
Zabuni. Aidha, viongozi wa Wizara ya Madini, Wizara ya Fedha, Viongozi
wa Mkoa wa Manyara, TRA na Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya mkoa wa
Manyara wanashirikiana kwa pamoja kuhakikisha kuwa mnada huo unafanyika
kwa ufanisi.
Aidha,
mnada huo utaiwezesha Serikali kupata mrabaha stahiki na kodi nyingine
ikiwa ni pamoja na tozo ya Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro.
Hadi
kufikia Desemba, 19,2017, zaidi ya wanunuzi 55 tayari wamejaza fomu za
kuwawezesha kushindana kwenye zabuni za kununua madini hayo,wakiwepo
watanzania 39 na wanunuzi 16 kutoka nje ya Tanzania
Kamishna
Mchwampaka alisema kuwa minada kama hiyo pia hufanyika kwa nchi za
Afrika zenye madini ya Vito kama vile Zambia( emerald), Zimbabwe (
Almasi) pamoja na Afrika kusini ( Almasi).