Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Hassan A. Ramadhan
(kulia) akifafanua jambo kwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu
(wa pili kulia) kuhusu mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
inavyosaidia kurahisisha mawasiliano na utendajikazi katika Ofisi ya Uhamiaji
Mkoa wa Kusini Pemba. Kamishna Sururu
akiendelea na ziara ya kikazi, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 – 19 Disemba,
2017.
Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Juma A. Khamis (aliesimama)
akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M.
Sururu (hayupo pichani) na Watumishi wa Idara ya Uhamiaji walioko Mkoa wa Kusini
Pemba leo tarehe 19 Disemba, 2017. Alisema “Ongezeko la Bandari Bubu ndani ya
Wilaya ya Mkoani ni changamoto kubwa katika utekelezaji wa majukumu yetu.
Tunazo takriban Bandari bubu 103, tunaomba Idara itupatie gari la kufanyia
doria katika maeneo hayo”. Kwa upande wake Kamishna Sururu katika ziara yake hiyo
ya kikazi Mkoani humo, aliahidi kulifanyia kazi ombi mapema iwezekanavyo.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu
(kushoto) akikagua baadhi ya magari chakavu yaliyopo katika Ofisi ya Uhamiaji
Mkoa wa Kusini Pemba, yanayosubiri kupigwa mnada baada ya kukamilika kwa
taratibu za uuzaji wa Mali za Serikali. Wakati wa ziara ya kikazi Mkoa wa
Kusini Pemba tarehe 18 – 19 Disemba, 2017. Pamoja na kutembelea maeneo mbali
mbali ya utendaji kazi Mkoani humo ikiwemo Bandari ya Mkoani, Bandari ya Wesha
iliyopo Chake Chake na Bandari bubu kadhaa. Kulia kwake ni Afisa Uhamiaji Mkoa
wa Kusini Pemba, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdi Bulushi.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu
akikagua kitabu cha utoaji wa Hati za Dharura za Kusafiria “ETD” katika Ofisi ya
Uhamiaji Wilaya ya Mkoani, zinazotolewa kwa Watanzania wanaohitaji kusafiri nje
ya Nchi. Huku akiwasisitiza Maofisa Uhamiaji katika utoaji wa Hati hizo wazingatie
vyema Sheria na Taratibu zilizopo ili kuepusha matumizi yasiyo sahihi. Aliyasema
hayo wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 – 19
Disemba, 2017. Hati za Kusafiria za Dharura ni miongoni mwa Hati mbali mbali za
Kusafiria zinazotelewa na Idara ya Uhamiaji Nchini
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu
akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi
ya bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia za Kengeja na Muwambe, Kusini
Magharibi mwa kisiwa cha Pemba, kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi na
kijamii, ambazo hutumika kama vipenyo kwa watu kuingia na kutoka visiwani humo
kinyume na taratibu za Uhamiaji. Wakati alipofanya ziara ya kikazi maeneo mbali
mbali ndani ya Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 Disemba, 2017.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akitoa
nasaha zake kwa Maafisa, Askari na watumishi Raia wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa
Kusini Pemba, wakati akihitimisha ziara ya kikazi Mkoani humo Leo tarehe 19
Disemba, 2017. Aidha, Kamishna Sururu aliwataka watumishi wote kuzingatia
maadili ya kazi, pamoja na kutilia mkazo matumizi sahihi ya mitandao ya
kijamii. “Naelewa tupo kwenye utandawazi, lakini narudia kuwasihi matumizi ya
Mitandao ya kijamii itumike kwa kuzingatia Kanuni na Miongozo ya Serikali, pia
mjiepushe na utoaji wa Siri na Taarifa za serikali, ni mwiko kutoa taarifa
yoyote. fuateni Sheria na Taratibu tulizowekewa”.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu
akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi
ya bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia za Kengeja na Muwambe, Kusini
Magharibi mwa kisiwa cha Pemba, kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi na
kijamii, ambazo hutumika kama vipenyo kwa watu kuingia na kutoka visiwani humo
kinyume na taratibu za Uhamiaji. Wakati alipofanya ziara ya kikazi maeneo mbali
mbali ndani ya Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 Disemba, 2017.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu
akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi
ya bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia za Kengeja na Muwambe, Kusini
Magharibi mwa kisiwa cha Pemba, kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi na
kijamii, ambazo hutumika kama vipenyo kwa watu kuingia na kutoka visiwani humo
kinyume na taratibu za Uhamiaji. Wakati alipofanya ziara ya kikazi maeneo mbali
mbali ndani ya Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 Disemba, 2017.
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, Naibu Kamishna wa
Uhamiaji, Abdi Bulushi akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M.
Sururu (wa pili kulia) na Maafisa Uhamiaji aliombatana nao, matunzo na usafi wa
mazingira katika nyumba za Makaazi ya Askari wa Uhamiaji, zilizoko eneo la
Ndugukitu, Wilaya ya Chake chake, Mkoa wa Kusini Pemba. Kamishna Sururu yupo
Mkoa wa Kusini Pemba kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 18 – 19 Disemba, 2018.
Aidha, Nyumba hizo zilifunguliwa rasmi na Mhe. Makamo wa Pili wa Rais, Balozi
Seif Iddi mapema mwezi Januari, 2017.
Mojawapo ya nyumba za Makaazi ya Askari wa Uhamiaji, zilizoko eneo la Ndugukitu, Wilaya ya Chake chake, Mkoa wa Kusini Pemba. Kamishna Sururu yupo Mkoa wa Kusini Pemba kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 18 – 19 Disemba, 2018. Aidha, Nyumba hizo zilifunguliwa rasmi na Mhe. Makamo wa Pili wa Rais, Balozi Seif Iddi mapema mwezi Januari, 2017.