KONGAMANO LA UTALII NA WANAHABARI NA WADAU WA UTALII KUFANYIKA JANUARI 19, ARUSHA

December 20, 2017
ANDREA NGOBOLE


Katibu mtendaji wa vyama vya waongoza watalii nchini (TTGA) Emmanuel Mollel akizungumza katika kongamano la utalii na kuiomba serikali kuondoa kero zao ikiwepo malipo duni na kutokuwepo kwa mtaala wa kitaifa wa waongoza utalii, kongamano hilo lilifanyika Arusha Palace Hotel.

Mratibu wa mradi wa jumuiko la maliasili Tanzania (TNRF) Jumapili Chenga akitoa mada katika kongamano la utalii kuhusiana na umuhimu wa hifadhi za jamii (WMA) katika uhifadhi nchini katika ukumbi wa Arusha Palace Hotel, kongamano hilo liliandaliwa na taasisi ya Arusha Media.

Afisa utalii katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha Flora Basir, akizungumza katika kongamano la utalii mkoani Arusha na kueleza jinsi serikali mkoani Arusha ilivyojipanga kuhakikisha mkoa wa Arusha inakuwa kitovu kikuu cha utalii barani Afrika, kwa kuondoa kero katika sekta ya utalii, kongamano hilo lilifanyika Palace Hotel kwa kuwashirikisha wanahabri na wadau wa utalii
Mratibu wa Tamasha hilo, Andrea Ngobole   katikati akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari awapo pichani
 NA: MWANDISHI WETU ARUSHA

Kongamano la pili la  utalii na amani ambalo hushirikisha wanahabari, wanafunzi  na wadau wa utalii nchini, linatarajiwa kufanyika  mkoani Arusha, Januari 19,2018.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mratibu wa kongamano hilo la pili kufanyika mkoani hapa, Andrea Ngobole alisema, kongamano  hilo, limeandaliwa na taasisi ya Arusha Media kwa kushirikiana na Shahanga sports promotion.

Ngobole alisema, lengo la kongamano hilo ni kuhamasisha utalii wa ndani na kupinga vita ujangili na kuhamasisha uhifadhi endelevu ambao utashirikisha jamii.
Alisema katika kongamano hilo,wanahabari watajadili mchango wa vyombo vya habari katika kukuza  utalii na  vita dhidi ya ujangili  pia umuhimu wa jamii kushiriki katika uhifadhi endelevu kwa maslahi ya taifa.

“kama ilivyokawaida mada mbali mbali zitatolewa na wahifadhi, watafiti katika masuala ya uhifadhi na utalii na pia waandishi wa habari waliobobea katika masuala ya uhifadhi  ”alisema.

Alisema kongamano hilo pia litaambatana na mashindano ya riadha ya Tourism Marathon ambayo pia yatafanyika Arusha kuhamasha utalii.
Mkurugenzi wa taasisi ya Alfredo  Shahanga promotion, Alfredo Shahanga  alisema wanariadha zaidi ya 200 wanatarajiwa kushiriki.
"kwa ujumla kongamano la mashindano hayo ni sehemu ya tamasha la Arusha tourism Festival  ambalo linatarajiwa kuwakutanisha wanahabari, wadau wa utalii na wanariadha "alisema
Wanahabari ambao watashiriki kongamano hilo ni kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini, Dar es Salaam, Mara na maeneo mengine yenye vivutio vya utalii.

Na haya ni baadhi ya matukio yaliyotokea katika kongamano la mwaka jana hapa mkoani Arusha

Mwenyekiti wa kamati ya amani mkoa wa Arusha(APET) Petro Ahham akimkabidhi kikombe cha ushindi  wa bonanza la amani na utalii mkoa wa Arusha,nahodha wa timu ya Kitambi Noma, James Lugangira lililofanyika vuwanja vya general tyre jijini arusha
Wanamichezo wa kitambinoma wakiwa wanashabikia ushindi mara baada ya kukabidhiwa kombe katika kiwanja cha General Tyre jijini Arusha

Katibu wa Kamati ya Olympic Taifa.Filbert Bayi akimkabidhi zawadi mwanariadha Fabian Joseph kwa kushika nafasi ya pili michuano ya Arusha tourism Marathon.zawadi ya 250,000

 
Washindi wa mashindano ya riadha ya utalii mita 5000,kuanzia kulia mshindi wa kwanza, Emmanuel GIriki, akifatiwa na Gabriel Geay na mshindi wa tatu Ismail Juma mara baada ya kumaliza mbio hizo katika uwanja wa sheikh Amri Abeid.
Washindi riadha mita 3000 la mashindano ya Utalii, wa kwanza kuanzia kulia, Angelina Tsere, wa pili Jackline Sakito na wa tatu Cesilia Gonoka jana baada ya kumaliza mbio hizo katika uwanja wa sheikh Amri Abeid.
Washiriki wa mashindano ya Utalii ya riadha yaliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mwezi January mwaka huu



Afisa Michezo Mkoa wa Arusha.Mwanmvita Okeng'o akimkabidhi zawadi ya kwanza Angelina Tsere baada ya kushinda Arusha tourism Marathon alizawadiwa sh 500,000.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »