Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais wa Msumbiji Filipe
Nyusi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Hassan Suluhu,Waziri Mkuu Mhe.Kassim
Majaliwa , Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe.Balozi Dkt.Augustine Mahiga ,Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga
Taifa Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Dkt
Bilinith Mahenge wakiwa uwanja wa Ndege wa Dodoma kumpokea Rais wa
Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi.
Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi
akishuka kutoka katika ndege iliyomleta katika uwanja wa ndege wa
Dodoma kwa ziara ya kikazi ya siku moja na kulakiwa na mwenyeji wake
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akimtambulisha Mgeni wake Rais wa
Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi kwa viongozi mbalimbali wa Serikali waliofika
katika uwanja wa Ndege wa Dodoma kumpokea.
Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi
akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi waliofika kumpokea
katika uwanja wa Ndege wa Dodoma kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji
Filipe Nyusi wakipita kwenye gadi ya Heshima iliyoandaliwa na Jeshi la
Wananchi mara baada ya Rais huyo wa Msumbiji kuwasili katika uwanja wa
ndege wa Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji
Filipe Nyusi wakati wakiangalia vikundi vya ngoma za utamaduni mara
baada ya Rais huyo wa Msumbiji kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mjini
Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mgeni wake Rais wa
Msumbiji Filipe Nyusi wakati vikundi vya ngoma vilipokuwa vikitumbuiza
katika uwanja wa ndege wa Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji
Filipe Nyusi katika Ikulu ya Dodoma kabla ya kuanza mazungumzo yao.
PICHA NA IKULU