Meneja wa Njia Kuu za Umeme,Mhandisi Amos Kaihula akitoa mada katika mkutano wa wanakijiji cha Misigiri mkoani Singida
Mkuu wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida,Emanuel Luhahula akizungumza
![]() |
Meneja wa Njia Kuu za Umeme,Mhandisi Amos Kaihula akizungumza na waandishi wa habari |
Meneja wa Njia Kuu za Umeme,Mhandisi Amos Kaihula akisisitiza jambo kwenye mkutano huo
WANANCHI wa kijiji cha Misigiri mkoani Singida wakifuatilia mkutano huo
Mmoja kati wa wananchi akiuliza swali katika mkutano huo
Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Misigiri mkoani Singida wakifuatilia mkutano huo
WANANCHI
wametakiwa kuithamini na kuitunza miundombinu ya umeme ambayo imewekezwa kwa
fedha nyingi ili kuhakikisha wanapata wanapata uhakika wa huduma ya umeme katika
maeneo yao yanayowazunguka.
Hayo
yalisemwa leo na Mkuu wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida Emanuel Luhahula
ambapo amesema kumekuwa na viashiria vya baadhi ya watu kuihujumu miundombinu
ya umeme kwa maslahi binafasi jambo ambalo kufanya hivyo kunaathiri upatikanaji
wa hudumaa hizo kwa wananchi.
“Lakini wanafanya
hivyo bila kuthamini jitihada kubwa zinazofanywa na serikali …Hawa ni
wanaoihujumu miundombinu ya umeme hawatavumiliwa hata kidogo kwa maana
wanarudisha nyuma jitihada za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais
JPM ambayo malengo yake makubwa ni kuinua uchumi wa wananchi kupitia viwanda ”Alisema.
Alisema
viwanda hivyo vinategemea umeme na ndio maana serikali imeamua kuwekea kwenye
nishati ya umeme hivyo watakaobainika
wamehusika kuharibu miundombinu watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.
Aidha
aliwaomba wananchi kushirikiana na serikali ikiwemo shirika la Tanesco
kuhakikisha miundombinu ya umeme iliyopo kwenye maeneo yao inatunzwa sanjari na
kuwafichua watu wote wenye nia ovu ya kurudisha nyuma maendeleo kwa kuihujumu.
Awali
akizungumza Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Polisi (OCD) Bw Kimolo alisema kuwa
kosa la uharibifu wa miundombinu ya umme ni sawa na lile la kuhujumu uchumi
hivyo wananchi wasilichukulie kama jambo la mzaha.
Alisema
uhujumu uchumi ni kosa kisheria hivyo wananchi wanapaswa kujihadhari na vitendo
vya uvunjifu wa sheria kwani serikali ipo macho kwa kushirikiana na wananchi
ili kuwafichua uhalifu huo.
Kwa upande
wake akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Misigiri
Mkoani Singida,Meneja wa Njia kuu za Umeme Mhandisi Amosi Kaihula alisisitiza
suala la utunzaji wa miundombinu kuwa ni jukumu wananchi wanaoishi kwenye
maeneo iliyopo kwani ni mali ya umma na shirika hilo limepewa dhamana ya
kuisimamia.
“Ubadhirifu
wa miundombinu hii una madhara makubwa ikiwemo kusababisha nchi kukosa umeme
lakini pia kupelekea matatizo ya kukatikakatika kwa huduma hiyo kwenye baadhi
ya maeneo jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya Taifa”Alisema.
Aliongeza
licha ya kurudisha nyuma maendeleo lakini pia kusababisha kukosekana kwa huduma
za kitabibu na kusimama kwa shughuli za viwanda
unaosababishwa na ukosefu wa umeme baada ya miundombinu kuhujumiwa.
Hata hivyo
aliwataka wananchi kushirikiana kuitunza miundombuni ya umeme ikiwemo kuachana na tabia za kufanya
shughuli za uchumi karibu na miundombinu ya umeme lakini wahakikishe wanachukua
tahadhari wanapoona nyaya za umeme zimeanguka au kuwepo kwa hitilafu yoyote ili
kuepuka ajali za umeme.