Baada
ya droo ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports
Federation Cup - ASFC), kukamilika Jumatano Desemba 06, 2017 kwenye
Studio za Kituo cha Televisheni cha Azam, kilichopo Tabata relini, Dar
es Salaam, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa ratiba
rasmi ya mechi hizo za raundi ya pili.
Kwa
mujibu wa TFF, michuano hiyo imepangwa kucheza kwa siku tano ambazo ni
Desemba 20, 21, 22, 23 na 24. Mchezo kati ya Simba na Green Warriors
utaochezwa Desemba 22, utakuwa ni maalumu kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa
michuano hiyo msimu. Sababu Simba ndiye bingwa mtetezi.
Ratiba hiyo iliyotolewa leo Desemba 12, 2017 inaonesha michezo ya Desemba 20, mwaka huu itakutanisha timu za JKT Mlale na KMC; Toto African ya Mwanza na Eleven Stars ya Kagera; Ambassador na JKT Oljoro; Boma
FC na Ndanda; Mvuvumwa na JKT Ruvu; Abajalo itakuwa mwenyeji wa
Tanzania Prisons wakati Milambo ya Tabora itacheza Buseresere ya Geita.
Desemba
21, 2017 Mshikamano itacheza na Polisi Tanzania; Rhino ya Tabora na
Alliance ya Mwanza; Majimaji Rangeres ya Lindi itapambana na Mbeya
Kwanza ya Mbeya; Njombe Mji na Mji Mkuu ya Dodoma; Ashanti na Friends
Rangers za Dar es Salaam; Kagera Sugar na Makambako wakati Stand United
ya Shinyanga itacheza na AFC ya Arusha.
Desemba
22, mwaka huu kutakuwa na mechi za Green Warriors na Simba; Polisi Dar
itapambana na Mgambo JKT ya Tanga; Kariakoo ya Lindi na Transit Camp ya
Dar ila kwa sasa imeweka maskani Shinyanga; Biashara ya Mara itacheza na
Mawenzi Market ya Morogoro; Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani
itacheza na Madini FC ya jijini Arusha huku Mufindi United na Pamba ya
Mwanza ilihali Singida United itacheza na Bodaboda FC.
Siku
ya Desemba 23, mwaka huu Azam FC itacheza na Area C; African Lyon ya
Dar es Salaam na Kiluvya United ya Pwani; Makanyagio itapambana na Mbao;
Mwadui na Pepsi; Majimaji na New Generation wakati Mbeya City itacheza
na Ihefu.
Desemba
24, 2017 Young Africans itacheza na Reha FC; Burkina ya Morogoro
na Lipuli ya Iringa; Coastal Union ya Tanga na Dodoma Fc ya Dodoma;
Shupavu na Real Mojamoja wakati Villa Squad itacheza na Mtibwa Sugar ya
Morogoro.
