NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mbeya
TAKRIBAN
madaktari na watoa huduma za afya 100 kutoka mikoa saba ya Kanada ya
Nyanda za Juu Kusini, wameanza kupatiwa mafunzo jijini Mbeya
yanayoratibiwa na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF).
Akizungumza
wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo ya siku tano yaliyofunguliwa
rasmi Desemba 12, 2017 (jana) NA Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makala
kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Mbeya, Mkurugenzi Mkuu wa WCF,
Bw.Masha Mshomba, alisema, mafunzo hayo ni muendelezo wa mafunzo kwa
madaktari na watoa huduma za afya ili kuwajengea uwezo wa kufanya
tathmini ya ulemavu maradhi anayopata mfanyakazi wakati akitekeleza
majukumu yake mahala pa kazi ili hatimaye madaktari hao waweze kutoa
mapendekezo kuwezesha mfuko kutoa mafao ya fidia stahiki.
Kwa
mujibu wa mratibu wa mafunzo hayo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma
za Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, mafunzo hayo
yamewaleta pamoja madaktari na watoa huduma za afya kutoka mikoa ya
Mbeya, Songwe, Katavi, Rukwa, Iringa, Njombe na Ruvuma.
Katika
hatua ya kuimarisha Hifadhi ya Jamii, Tanzania, Serikali ilianzisha
Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi kwa mujibu wa kifungu namba 5 cha sheria
ya Fidia kwa Wafanyakazi, kipengele cha 263 kilichofanyiwa marejeo
mwaka 2015 ili kuhakikisha kila mfanyakazi Tanzania Bara kutoka sekta ya
umma na binafsi anapata fursa ya kuwekewa bima na mwajiri wake ili
anapopata majeraha au magonjwa awapo kazini basi aweze kufidiwa kwa
mujibu wa sheria, alisema Bw. Mshomba.
“Lengo
kuu la kuanzishwa kwa Mfuko huu ni kutoa fidia stahiki kwa mfanyakazi
aliyepatwa na majeraha, maradhi kutokana na kutekeleza wajibu wake awapo
kazini, lakini pia kuwalipa fidia wategemezi wake anapofariki katika
mazingira hayo.” Alifafanua Bw. Mshomba na kuongeza, WCF ilianza
kutekeleza majukumu yake Julai Mosi, 2015 na mwaka uliofuata Mfuko
ulianza rasmi kupokea madai ya fidia na kulipa mafao kwa waathirika.
Wakati
akifungua Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa WCF jijini Arusha
mwishoni mwa mwezi uliopita, kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira
na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, aliitaka WCF kuendelea
kutoa elimu kwa wadau, ili waweze kuelewa vema shughuli za Mfuko na nia
njema ya serikali ya kuanzisha mfuko huo ili mfanyakazi wa Tanzania
aweze kupata fidia stahiki anapopata madhara sehemu ya kazi.
Bw,
Mshomba aliishukuru Serikali na Wizara zake kwa kuunga mkono na
kusaidia juhudi za WCF katika kuimarisha mifumo yake ili kutoa huduma
bora kwa wadau wake.“Pia
napenda nizishukuru taasisi za Hospitali ya Taifa Muhimbili, MOI, Ocea
Road Hospital, MUHAS, na OSHA kwa kuwaruhusu wataalamu wake ili
tuwatumie katika kutoa mafunzo haya.” Alisema.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Amos Makala ambaye alikuwa
mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo, alisema, juhudi za
ushirikiano wa pamoja miongoni mwa wadau yaani Serikali, Wafanyakazi,
Waajiri unahitajika sana kuhakikisha tathmini endelevu ili kuimarisha
mfuko.
“Nimeambiwa
mafunzo haya yataongeza uelewa katika kufanya tathmini na uchunguzi wa
majeraha au maradhi anayoyapata mfanyakazi mahala pa kazi na kutoa
mapendekezo stahiki kwa uamuzi wa mwisho.” Mkuu
wa Mkoa pia alipongeza juhudi za WCF kwa kuendesha mafunzo hayo ambayo
yatawezesha kupanua wigo wa mtandao wa watoa huduma za afya na
hospitali
“Katika
mwaka wa fedha wa 2015/2016 naambiwa mlianza kutoa mafunzo kwa
madaktari na watoa huduma za afya wapatao 359, katika wailaya zote za
Tanzania Bara mafunzo mliyoyaendesha katika kanda nne za Pwani, kanda ya
Ziwa, kanda ya Kaskazini, na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na mwaka
uliofuata mkatoa mafunzo kwa madaktari wapatao 145 katika mikoa ya Dar
es Salaam na Mwanza na kufanya idadi ya jumla hadi sasa ya madaktari na
watoa huduma za afya ambao mmewapatia mafunzo kufikia 504, napenda
kuipongeza Bodi ya Wadhamini na uongozi wa Mfuko kwa kazi nzuri
mnayofanya.” Alimaliza Mkuu wa Mkoa Bw. Amos Makala.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makala, akihutubia wakati akifungua rasmi
mafunzo ya siku tano kwa madaktari wanaofikia 100 kutoka mikoa saba ya
kanda ya nyanda za juu Kusini, kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa, jijini
humo Desemba 12, 2017. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi, (WCF), yanalenga kuwajengea uwezo madaktari na watoa
huduma za afya kufanya tahmini ya mfanyakazi aliyepata ulemavu au
ugonjwa mahali pa kazi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfukom wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba,
akitoa hotuba ya ukaribisho kweye ufunguzi rasmi wa mafunzo ya siku tano
kwa madaktari wanaofikia 100 kutoka mikoa saba ya kanda ya nyanda za
juu Kusini, kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa, jijini humo Desemba 12,
2017. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na WCF, yanalenga kuwajengea uwezo
madaktari na watoa huduma za afya kufanya tahmini ya mfanyakazi
aliyepata ulemavu au ugonjwa mahali pa kazi. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya, Mhe. Amos Makala, na Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa Mfuko huo,
Dkt. Abdulsalaam Omar.
Washiriki wakifuatilia hotuba kwa umakini.
Washiriki wakifuatilia hotuba kwa umakini.
Washiriki wakifuatilia hotuba kwa umakini.
Mshiriki akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Dkt. Ali Mtulia(kushoto) kutoka WCF, na wawezeshaji wakifuatilia hotuba hiyo.
Washiriki wakifuatilia hotuba kwa umakini.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kungenge, akiwa makini kufuatilia hotuba.
Sekretariat
ya WCF ikiwa kwenye majadiliano ili kuhakikisha mafunzo yanakwenda kwa
ufasaha. Kutoka kushoto ni Dkt. Pascal Magesa, Bw.Vincent Steven, Bi.
Laura Kunenge, na Bi.Innocencia William.
Afisa Kazi Mkoa wa Mbeya, Bi. Mary Patrick Mwansisya (kulia na maafisa wengine wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa.
Bw. Mshomba akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makala wakati akihutubia madaktari.
Mhe. Makala, akionyesha kitu, akiwa Bw. Mshomba
Picha ya pamoja kundi la kwanza
Picha ya pamoja kundi la kwanza
Picha ya pamoja kundi la kwanza
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Amos Makala, (kushoto), akipongezwa na
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha
Mshomba, (kushoto) mara baada ya kutoa hotuba yake ya ufunguzi rasmi wa
mafunzo ya siku tano kwa madaktari wanaofikia 100 kutoka mikoa saba ya
kanda ya nyanda za juu Kusini, kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa, jijini
humo jana (Desemba 12, 2017). Mafunzo hayo yanayoratibiwa na WCF
yanalenga kuwajengea uwezo madaktari na watoa huduma za afya kufanya
tahmini ya mfanyakazi aliyepata ulemavu au ugonjwa mahali npa kazi.
Mafunzo hayo yanafanyika jijini Mbeya.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Amos Makala, (kulia), akiongozana na
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, 9WCF), Bw. Masha
Mshomba, baada ya ufunguzi rasmoi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktari
wanaofikia 100 kutka mikoa saba ya kanda ya nyanda za juu Kusini, kwenye
ukumbi wa Benjamin Mkapa, jijini humo. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na
WCF yanalenga kuwajengea uwezo madaktari na watoa huduma za afya kufanya
tahmini ya mfanyakazi aliyepata ulemavu unaotokana na ajali au magonjwa
mahala pa kazi