TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAKE JUU YA MFUMO WA UNUNUZI WA LUKU

December 10, 2017
 Na Humphrey
Shao, Globu ya Jamii
 
Shirika la
Umeme Tanzania Tanesco limewatoa hofu wateja wake juu ya mfumo wa ununuzi wa
Umeme kwa njia ya luku na kusema kuwa kwa sasa upo sawa na wanaweza kununua
katika mifumo iliyozoeleka.
 
Akizungumza
mapema leo jijini Dar es Salaam Kaimu Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano(TEHAMA)
wa Tanesco, Demetruce Dashina amesema
kuwa kulitokea tatizo dogo la mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya Luku
kutokana na wataalamu wa shirika hilo walipokuwa wakiamisha mitambo hiyo kutoka
ofisi ya Zamani kwenda sehemu nyingine.
 
“Jana
tulikuwa tunafanya uhamisho wa mfumo wa luku kwende katika ofisi zetu mpya hivyo
ikawalazimu wateja wetu kupata usumbufu kidogo, lakini kuanzia saa saba mfumo
huo umekaa sawa na wateja wanaweza kununua umeme kama walivyokuwa wanafanya
hapo awali bila shida yoyote mara baada ya marekebisho ya kiufundi” amesema
Dashina
 
Amesema kuwa
shirika lilijipanga kuwahudumia wateja wake kama kawaida wakati wa kuhamisha
mitambo hiyo lakini Wananchi wengi wakapata taharuki hivyo kufanya mfumo wa
ziada kuzidiwa kutokana na watu kununua umeme kuliko Kawaida.
Kwa upande
wake Kaimu Meneja  Uhusiano wa Tanesco Leila Muhaji amewaomba radhi wananchi kwa
usumbufu uliojitokeza na kuwasisitiza kuwa sasa wanaweza kununua katika mifumo
iliyozoeleka.
 
Muhaji
amesema kuwa Tanesco inatambua umuhimu wa umeme hivyo 
  kuwataka watanzania kuwa na Imani na shirika lao kwani lipo kwa ajili ya
kuwahudumia  kama inavyohitajika.
 Kaimu
Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano(TEHAMA)
 wa Shirika la Umeme nchini Tanesco, Demetruce Dashina Akizungumza na Waandishi mara baada ya kuimarika kwa mfumo wa kununua Umeme kwa njia Luku 
   Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco, Leila Muhaji akifafanua jambo wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari juu ya kuimarika kwa Mfumo wa Ununuzi wa luku mara baada ya kuhamia sehemu nyingine. 
Waandishi wa habari habari walifika katika mkutano huo wakifatilia kwa Makini.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »