Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa
kilele cha maadhimisho ya siku Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa
kwenye Viwanja vya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Ndugu Rodgers
William Sianga wakati akiwasili kwenye kilele cha maadhimisho ya siku
Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa kwenye Viwanja vya kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Bahame Tom
Nyanduga (kulia) alipotembelea banda lao wakati wa kilele cha
maadhimisho ya siku Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa kwenye Viwanja
vya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mjini Dodoma.
Sehemu ya wahudhuriaji wa kilele
cha maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa
yaliyofanyika kwenye viwanja vya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mjini
Dodoma
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
……………
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
ameziagiza Taasisi zote zenye usimamizi kuhakikisha zinasimamia vyema
jukumu lao la kutumia nafasi zao kuongeza juhudi katika kuimarisha
misingi ya Utawala Bora, Uwazi, Uadilifu na Uwajibikaji.
Makamu
wa Rais aliyasema hayo leo wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya siku ya
Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa yaliofanyika kwenye uwanja wa
kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mjini Dodoma.
Makamu
wa Rais alisema Vita dhidi ya ukiukwaji wa Maadili haiwezi kupiganwa na
Serikali peke yake, “Ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kuwa
vitendo vya rushwa, ubadhirifu na maovu mengine vinatokomezwa”
Serikali
ya Awamu ya Tano itaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kisera na
kisheria ambayo itahakikisha vijana wanakuzwa kimaadili kwani hakuna
Taifa Duniani linaweza kupata maendeleo bila kuwa na utamaduni
unaozingatia maadili alisema Makamu wa Rais.
Makamu
wa Rais alisisitiza kuwa ili kujenga Utawala Bora ni lazima kuweka
uwiano wa yanayofanyika na serikali kuu hadi serikali ya mitaa nchi
nzima.Serikali ilizindua Rasmi mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na
Mpango wa Utekelezaji Awamu ya Tatu (NACSAP III) Desemba 2016.
Makamu
wa Rais alisema kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa baadhi ya
Ofisi za Serikali, Serikali imeamua kufuatilia uhalali wa vyeti vya
Watumishi, Idadi halali ya Watumishi wa Umma na ulipaji wa Mishahara
Hewa na kusisitiza zoezi ili litakuwa endelevu.
Mwisho,
Makamu wa Rais aliwaeleza wananchi na Watumishi wa Umma kwa ujumla kuwa
Maadili ni nguzo muhimu katika maendeleo ya nchi yetu. “Ni imani
yangu kuwa Wakuu wa Taasisi hizi kuwa mtahakikisha misingi ya haki za
binadamu, utawala bora na viwango vya Maadili ya Viongozi wa Umma
vinasimamiwa ipasavyo ili kuimarisha nidhamu ya Maafisa na Watumishi wa
Umma”.
Kuimarishwa
na kudumishwa kwa nidhamu ya utendaji, huduma zitolewazo Serikalini,
Ukusanyaji wa mapato na matumizi bora ya fedha za Serikali kutaleta
mafanikio katika kuelekea uchumi wa kati.