Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB) ametoa mud wa
siku 30 kwa wahusika ambao ni wamiliki wa magogo yaliyokamatwa katika
bandari ya Dar e s Salaam (TPA) ambayo yalikuwa yasafirishwe nje ya
Nchi, kujitokeza haraka kueleza wameyato wapi na walikuwa na lengo gani
baada ya kuyatelekeza bandarini hapo kwa muda wa miaka 10 sasa huku
mengine yakitelekezwa pasipo kuwa na vibali maalum.
Dk.Kigwangalla
ametoa kauli hiyo baada ya kufanya ziara ya ghafla bandarini hapo
kukagua mali na bidhaa zinazoshughulikiwa na Wizara yake hiyo ambapo
katika zkukagua kwake huko alibaini uwepo wa makontena hayo 55 ambayo
yapo kwa miaka 10 sasa yakihifadhiwa huku wahusika wakishindwa
kujitokeza.
“Naagiza
mamlaka zilizo chini ya wizara yangu kuhakikisha wanahakiki magogo yote
yalipo hapa bandarini. Mwenye huu mzigo lazima ajulikane hasa haya
magogo 938, Ndani ya siku 30 mwenye haya magogo atangaziwe na ajitokeze
vinginevyo itabaki kuwa mali ya Serikali” alisema Dk. Kigwangalla.
Hata
hivyo aliagiza pia kontena 55 zilizokutwa bandarini hapo zenye magogo
pia nazo wahusika wajitokeze na nyaraka zao kamili ili waeleze kama
kweli wameyatoa Zambia magogo hayo ama sehemu gani hivyo wajitokeze na
wasipofanya hivyo ndani ya siku hizo 30, magogo hayo yatataifishwa na
kuwa mali ya Serikali.
Katika
ziara hiyo, Waziri Dk.Kigwangalla aliweza kutembelea bandari ya Dar es
Salaam pamoja na maeneo yanayohifadhiwa magogo hayo zikiwemo bandatri ya
nchi kavu ya NASACO, Malawi (Malawi Cargo) na baadae eneo hilo la
bandari ya Dar es Salaam.
Akiwa
katika eneo la Malawi Cargo, Waziri Dk. Kigwangalla aliweza kushuhudia
makontena mbalimbali yakiwemo yale ya mbao aina ya mitiki ambayo
inatarajiwa kusafirishwa nje ya nchi huku akibaini uwepo mkubwa wa
udanganyifu kwa wasimamizi wa upakuaji na usafirishaji katika eneo hilo
la bandari ambao awali walitaja idadi ndogo ya makontena ya mbao mbele
ya Waziri hali iliyopelekea kuanza kuyakagua makontena yote ndani ya
eneo hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangallaakitoa maagizo kwa uongozi wa bandari ya TPA.
Baadhi ya magogo hayo yaliyokutwa katika makontena bandarini hapo
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla wakiwa katika eneo
la bandari ya nchi kavu ya Malawi Cargo. wakati wa kukagua magogo hayo
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya
mbao zilizokutwa bandarini hapo katika eneo la Malawi Cargo
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya
mbao zilizokutwa bandarini hapo katika eneo la Malawi Cargo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akionyeshwa nyaraka ya idadi ya makontena katika eneo la Malawi Cargo
Zoezi la ukaguaji likiendeleaBaadhi ya magogo yaliyokutwa bandarini hapo
EmoticonEmoticon