WAVIU WASHAURI WATEMBELEA VITUO VIKUBWA VYA CTC HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO NA SEKOTOURE JIJINI MWANZA

December 03, 2017

Waviu Washauri kutoka mkoa wa Mwanza wametembelea vituo vikubwa vya tiba na matunzo katika hospitali ya Rufaa ya Bugando na Sekotoure jijini Mwanza ili kujifunza kwa kuona huduma mbalimbali zinazotolewa katika maeneo hayo.
Waviu washauri ni watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na wamejiweka wazi na huru kuwashauri watu wanaoishi na VVU kuhusu mambo mbalimbali ya afya ikiwemo ufuasi mzuri wa dawa, kutoa ushauri nasaha,kufundisha kwa njia ya ushuhuda wa maisha yao na kuhamasisha Waviu kujiunga katika vikundi ili kusaidiana na kupunguza unyanyapaa.
Lengo la mafunzo hayo kwa njia ya matembezi (Field Trip) ni kuwawezesha Waviu washauri kupata ubunifu wa kuboresha huduma mara watakaporudi kwenye maeneo yao ya kazi.
Miongoni mwa mambo waliyojifunza katika ziara hiyo iliyofanyika Novemba 30,2017, ni kuhusu utaratibu mzima wa utunzaji kumbukumbu,mtiririko wa huduma tangu mteja anapoingia hadi anatoka,njia mbalimbali za kukabiliana na wateja watoro na wapitaji,utoaji wa elimu sahihi ya VVU na Ukimwi na matumizi sahihi ya dawa na lishe bora. 
Jumla ya Waviu washauri 63 kutoka halmashauri za wilaya za Ilemela,Kwimba,Magu,Buchosa,Misungwi,Sengerema na Nyamagana wamekutana jijini Mwanza katika warsha ya siku tatu iliyoanza Novemba 28,2017 hadi Novemba 30,2017 kwa ajili ya kujengewa uwezo wa namna ya kuboresha huduma katika vituo vya tiba na matunzo (CTC). 
Warsha hiyo iliandaliwa na Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na huduma zinazohusiana na Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI katika mikoa ya Shinyanga,Simiyu,Mwanza,Geita,Tanga na Mara kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia shirika la Centres for Disease Control and Preventation (CDC).
Warsha hiyo imemalizika siku moja kabla ya siku ya Ukimwi duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Disemba Mosi na kauli mbiu ya mwaka huu ni 'Changia mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi nchini uokoe maisha - Tanzania bila Ukimwi inawezekana'.
ANGALIA HAPA CHINI MATUKIO WAKATI WA ZIARA YA WAVIU WASHAURI KATIKA HOSPITALI YA BUGANDO NA SEKOTOURE 
Kushoto ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona akitambulisha Waviu washauri waliotembelea hospitali ya rufaa Bugando jijini Mwanza kwa ajili ya kujifunza kwa kuona huduma mbalimbali zinazotolewa katika maeneo hayo. Katikati ni mtoa huduma za afya katika kituo cha tiba na matunzo katika hospitali ya Rufaa ya Bugando Shija Mashimba. Kulia ni Muuguzi Kiongozi kitengo tiba na matunzo katika hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, Sarah Bipa. 
Muuguzi Kiongozi kitengo tiba na matunzo katika hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, Sarah Bipa akielezea kuhusu namna wanavyopokea wateja na kuwahudumia.
Muuguzi Kiongozi kitengo tiba na matunzo katika hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, Sarah Bipa akisalimiana na waratibu wa huduma za afya ngazi ya jamii walioambatana na Waviu washauri waliotembelea hospitali hiyo. 
Sarah Bipa akizungumza na Waviu Washauri waliotembelea hospitali hiyo. 
Hapa ni katika eneo la wateja wanakaa kusubiri huduma: Kulia ni Sarah Bipa akielezea namna wanavyohudumia wateja,wanavyotoa elimu ya VVU/Ukimwi,elimu ya lishe bora na ufuasi mzuri wa dawa. 
Sarah Bipa akionyesha Waviu washauri namna wanavyotunza mafaili ya wateja katika hospitali hiyo. 
Sarah Bipa akiwa na Waviu Washauri katika chumba cha vipimo mbalimbali kama vile uzito na urefu. 
Sarah Bipa akiendelea kuwatembeza wageni wake katika maeneo mbalimbali ya hospitali ya rufaa Bugando. 
Hapa ni ndani ya chumba cha ushauri: Pichani ni Muuguzi Mshauri katika hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, Celina Katakomela akielezea namna wanavyotoa elimu kwa wateja kabla ya kuanza kutumia dawa. 
Ndani ya chumba cha dawa : Pichani ni dawa zinazofubaza makali ya VVU. 
Waviu washauri wakifuatilia maelezo kutoka kwa Sarah Bipa. 
Sarah Bipa akiendelea kuwatembeza wageni wake. 
Hapa ni katika hospitali ya Sekotoure jijini Mwanza: Kulia ni mtoa huduma za afya katika kituo cha tiba na matunzo hospitali ya Sekotoure,Bernadeta Luhende akionyesha kitabu cha kutunzia kumbukumbu za wateja. 
Mtoa huduma za afya katika kituo cha tiba na matunzo katika hospitali ya Sekotoure,Heri Abdul akielezea namna wanavyofuatilia wateja watoro. 
Muuguzi Kiongozi katika hospitali ya Sekotoure jijini Mwanza, Flora Masanja akionesha kitabu kwa ajili ya kufuatilia wateja watoro. 
Muuguzi Kiongozi katika hospitali ya Sekotoure jijini Mwanza, Flora Masanja akizungumza na Waviu Washauri.Alisema wastani wa wateja 80 hufika katika hospitali hiyo kila siku. 
Muuguzi Kiongozi katika hospitali ya Sekotoure jijini Mwanza, Flora Masanja akionyesha Waviu namna ya kujaza taarifa za wateja. 
Mtoa huduma za afya katika kituo cha tiba na matunzo katika hospitali ya Sekotoure, Heri Abdul akionyesha mafaili yanayotumika kutunzia kumbukumbu za wateja wanaofika katika hospitali hiyo. 
Mratibu wa watoa huduma za afya ngazi ya jamii mkoa wa Mwanza, Bi. Esperance Makuza, aliyemwakilisha Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mwanza akifunga warsha ya siku tatu ya Waviu washauri mkoa wa Mwanza katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jijini Mwanza Novemba 30,2017.
Waviu washauri wakimsikiliza Bi. Esperance Makuza wakati akifunga warsha hiyo.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »